ORODHA YA WANAWAKE WAREMBO MAARUFU WALIOFANIKIWA MWAKA JANA 2015.
10.SHAKIRA,mwanamuziki huyu wa colombia ambaye yupo kwenye uhusiano na beki wa kati wa barcelona Gerald Pique anashika namba 10 katika orodha hii.Licha ya kuwa mwanamuziki Shakira pia ni mwalimu wa kucheza,mwaka 2014 shakira aliweka rekodi ya kuwa mtu mwenye wafuasi wengi facebook,akiwa na wafuasi zaidi ya milioni 100.
9.PRIYANKA CHOPRA,ni mmoja kati ya waigizaji wanaolipwa pesa nyingi zaidi bollywood,mwaka huu na mwaka jana anaendelea kufanya vizuri na series ya quantico.katika orodha hii anashika namba 9.
8.KATE UPTON,Mwaka juzi alikuwa nafasi ya 8 pia katika jarida la people magazine alichaguliwa katika orodha ya wasichana wenye mvuto zaidi duniani.Kate ni mwanamitindo anayefanya vizuri duniani.
7.TAYLOR SWIFT,Taylor amefanikiwa sana kwa mwaka jana na kufanya hadi mwaka huu ashinde GRAMY,Licha ya Gramy taylor ana tuzo kibao kama za Billboard awards,academy awards,british awards,mtv awards na nyinginezo pia kauza zaidi ya nakala milioni 40 ya albam yake.
6.GAL GADOT,Aliwahi kuwa Miss Israel,Gal ni mwanamitindo akifanya kazi zake kupitia kampuni ya castro pia anajulikana sana kutokana na uwepo wake katika mfululizo wa filamu za fast and furious.
5.EMMA WATSON,Anajulikana zaidi kupitia filamu za harry porter,emma kwa mwaka jana alikuwa wa kwanza kwenye orodha ya Top 99 outstanding women of 2015,iliyoandaliwa na AskMen.Pia alishika nafasi ya 26 katika orodha ya watu wenye ushawishi zaidi duniani iliyoandaliwa na jarida la TIME.
4,CANDICE SWANAPOEL,Ni mwanamitindo toka South Africa,mwaka jana aliingia katika orodha ya wanawake warembo zaidi duniani,pia anashika nafasi ya 10 katika orodha ya wanamitindo wanaolipwa pesa nyingi zaidi duniani,orodha hiyo iliandaliwa na jarida la forbes.
3.DEEPIKA PADUKONE,Katika orodha hii anashika nafasi ya tatu,kashawahi kuingia kwenye orodha nyingi mbali mbali zinazohusu wanawake warembo,pia Deepika analipwa pesa nyingi sana kutokana na kazi zake za uigizaji pande za bollywood.
2.JENNIFER LOPEZ,Akiwa na zaidi ya miaka 40 Jennifer bado hajapoteza mvuto,Anaingiza pesa kupitia kazi zake za uigizaji,muziki na vipindi vya televisheni.Pia ana shughuli nyingine nyingi za kijasiriamali pamoja na foundation.
1.SHAILENE WOODLEY,anashika namba moja katika orodha hii,anajulikana kupitia kazi zake za filamu kama vile, The fault on our stars,Divergent na Descendants.Ni mmoja kati ya mabinti wadogo lakini wenyev mafanikio makubwa hollywood.
No comments: