Breaking News
recent

EDDIE MURPHY VS JOHN DEPP.


Kama unapenda Movies hakika jina John Depp halitakuwa ngeni masikioni kwako,kafanya movies nyingi sana lakini anajulikana sana kupitia jina la captain jack sparrow alilolipata kupitia movie ya PIRATES OF CARIBEAN.John Depp anasifika kuwa mkali wa kuvaa uhusika tofauti tofauti na huwa anabadilika sana katika kila movie anayofanya.hapo chini ntakuonyesha baadhi ya uhusika aliowahi kuuvaa John Depp Katika movies mbali mbali.
BAADHI YA UHUSIKA ALIOWAHI KUUVAA JOHN DEPP KATIKA MOVIES MBALI MBALI.
John Depp huwa anabadilika sana katika movies mbali mbali,mara awe mtu mpole,mara awe mkatili,kichaa,mkorofi yani uhusika wowote ule you name it yeye anauvaa na ukakufanya usahau kabisa kuwa ndiye yeye aliyekuwepo kwenye movies huko nyuma,na katika actors naowaheshimu Hollywood John naye yupo katika list,jamaa huwa anatendea haki movies kila akipewa uhusika flani auvae.
JOHN DEPP KATIKA MOVIE YA EDWARD AND THE SCISSORS HANDS.


JOHN DEPP KATIKA MOVIE YA INTO THE WOODS

JOHN DEPP KATIKA MOVIE YA THE BLACK MASS
JOHN DEPP KATIKA MOVIE YA ALICE IN THE WONDERLAND
JOHN DEPP KATIKA MOVIE MBALI MBALI KAMA PIRATES OF CARIBEAN,THE LONE RANGER N.K
Kwa jina moja John Depp ni master of disguise kutokana na ukweli kuwa huwa anavaa uhusika wa watu mbali mbali na kuumudu vyema,lakini John Depp hayupo peke yake HOLLYWOOD mtu mwingine mwenye mambo kama ya John Depp ya kuvaa uhusika kibao katika movie moja au tofauti ni Eddie Murphy hebu naye tumcheki hapo chini..
Eddie Murphy na yeye huwa anauvaa uhusika tofaauti tofauti kama John Depp lakini tofauti ni kuwa Eddie ni comedian John Depp hufanya movie yoyote ile ila Eddie mara nyingi huwa movie anayofanya hawi serious,Eddie kashafanya movies nyingi kama vile COMING TO AMERICA,DR DO LITTLE,A THOUSAND WORDS na NORBIT,Kwa hapa Bongo Eddie ni kama Joti naye huwa anavaa uhusika tofauti tofauti ndani ya movie moja anakuwa mtoto,kijana,babu,mama yani kila uhusika Eddie anauvaa na anautendea haki.
WAHUSIKA MBALI MBALI AMBAO EDDIE MURPHY ALIVAA KATIKA MOVIE YA THE NUTTY PROFESSOR..
EDDIE ALIVAA WAHUSIKA SITA KATIKA MOVIE YA THE NUTTY PROFESSOR.
EDDIE ALIUVAA UHUSIKA WA WATU WATATU KATIKA MOVIE YA NORBIT.
WAHUSIKA WOTE HAO HAPO JUU NI EDDIE MURPHY KATIKA MOVIE YA COMING TO AMERICA
Sio Eddie na John Tu wanaofanya multiple roles Hollywood,Wapo wengi na list yao nitakuletea siku nyingine ila hawa wawili ndio wapo on top of their game.......STAY TUNED FOR OUR UPCOMING POSTS.....Tchaoooo....,

No comments:

Powered by Blogger.