Breaking News
recent

WAJUE STALKERS WALIOSUMBUA MASTAR WA HOLLYWOOD.

Hivi ushawahi kufikiri kuwa kuna mtu anakupenda sana lakini wewe hujui, labda ni class mate wako,au ni co-worker au ni jirani yako,tunapenda kuwaita secret admires ,utakuta unapata barua kutoka kwake lakini hataki kujitambulisha kwako...sasa kuna hawa stalkers ,hawa ni wale watu wanaokuwa wanampenda au kumkubali sana mtu fulani kiasi kwamba huwa wanamfuatilia sana karibia kila kitu anachofanya mtu.Hawa jamaa huwa anakufuatilia na hata barua anakutumia huku akikutisha ,huwa wanafuatilia maisha ya watu  mpaka wanageuka tishio katika maisha ya mtu fulani...definition ya stalker ni hiyo hapo chini;
Definition ya neno stalking.
Kwa Celebrities nchini Marekani wamekumbana sana na stalkers,mastar wenye majina makubwa kama vile Beyonce,Miley Cyrus,Justin Bieber na wengineo tayari wameshakuwa victims wa stalkers.
Britney,Justin na  Miley ni baadhi ya celebrities waliosumbuliwa na stalkers.
 Wafuatao ni baaadhi ya stalkers waliosumbua sana celebrities wa Hollywood wengine walifikia kiasi cha kuhatarisha maisha ya mastar kutokana na vitisho vyao;
1-JASON LUIS RIVER stalker wa MILEY CYRUS.
 ''Mimi ni rafiki wa Miley Cyrus ,yeye ni mke wangu tumekuwa marafiki kwa muda wa miaka mitano sasa''  haya ni maneno aliyokuwa anayatamka Jason walipomkamata akijaribu kuiingia nyumbani kwa Miley huku akiwa na pea ya mkasi mkononi,Miley alimshitaki huyu jamaa,na akahukumiwa kifungo cha mies 18.
2-BASSEY ESSIEN stalker wa BEYONCE.

Bassey alikuwa anaamini kuwa Beyonce halisi amekufa na Beyonce tunayemfahamu ni fake anaishi maisha ya Beyonce halisia ambaye amefariki,jamaa alituma barua kadhaa kumtisha Beyonce kuwa aache kuishi maisha ya mtu mwingine,huyu jamaa alisumbua sana mpaka Beyonce alipokwenda kufanya show London alitoa tahadhari kwa watakaolinda kuwa wawe waangalifu ikitokea jamaa angevamia katika show,issue yote hii ilitokea mwaka 2009.
3-KAREN McNEIL stalker wa JUSTIN TIMBERLAKE

Huyu Karen alienda nyumbani kwa Justin Timberlake, Los Angeles akidai kuwa yeye ni Mungu,eti yeye na JT wataitawala dunia,Karen alikamatwa na polisi na wakaamua kumpeleka hospitali ili wakamcheck akili.
4-MASAHIKO SISAWA stalker wa BRITNEY SPEARS.
Masahiko alikuwa anampenda sana Britney na mara nyingi alikuwa anamfuatilia hadi nyumbani kwake,alikuwa akituma barua kwa Britney pamoja na e-mails,pia alikuwa akimtumia Britney picha kadhaa na massage iliyoandikwa ''am chasing you'',baadae jamaa alishitakiwa na akapewa amri na mahakama ya kukaa mbali na Britney ''restraining order'' lakini hakujali aliendelea kumsumbua,baadae naye Masahiko aliamua kumshitaki Britney kwa kuwa Bodyguards walimtishia bastola,kesi haikudumu sana mahakamani wakaivungia,issue hii ilitokea mwaka 2002.
5-DANA MARTIN,MARK STAAKE na TANNER LUANE stalkers wa JUSTIN BIEBER.
Dana Martin ni jamaa aliyekuwa anatumikia kifungo cha maisha katika jela ya New Mexico,kwa kosa la kumbaka na kumuua binti wa miaka 15,Dana alitokewa kuvutiwa na JB hivyo akaongea na rafiki yake waliyefungwa wote Mark Staake na binamu wa Mark Staake ambaye ni Tanner Luner kuwa amtafute Justin Bieber akipatikana akatwe korodani  alafu aletewe yeye huko jela..[hahaha huyu alitoa mpya],lakini baadaye kabla hata hawajakamilisha mpango huu Mark na Tanner walikamatwa.
6-THOMAS BRODNICK Stalker wa SELENA GOMES.
Huyu jamaa alisema eti kaongea na Mungu mara hamsini akipewa amri kuwa amuue Selena,ilikuwa ni mwaka 2011 kituko hiki kilipotokea, Brodnicki aliamua kumuomba Selena kuwa amuwekee amri kutoka mahakamani itakayomtaka akae mbali na selena ''restraining order''alisema hiyo ndiyo njia pekee ambayo itamfanya asimfuatilie Selena asipofanya hivyo basi atamuua.Mwaka 2012 Selena alimuwekea Brodnicki ''restraining order'' ya miaka mitatu.
7-ROBERT DEWEY HOSKINS stalker wa MADONNA.

Huyu jamaa ni psychopath kwani toka miaka ya 90 alifungwa kwa kosa la kum-stalk Madonna,lakini mwaka 2012 alitoroka hospitali ya vichaa ambapo ndipo alipofungiwa,jamaa alisema nia yake ni moja tu either amuoe Maddona au kama akikataa basi atamuua,licha ya kutoroka Robert alifanikiwa kukamatwa na  kurudishwa hospitali ya vichaa.
 8-JOHN M. DUBIS Stalker wa JENNIFER LOPES.
J.LO naye alijikuta matatani baada ya jamaa anayeitwa John M. Dubis Kuvamia nyumbani kwake na kujificha kwa muda wa siku sita bila kugundulika na mtu,baadae huyu mtu alikamatwa na akawekewa ''restraining order'' ili asije tena kumsumbua J.LO.
 
Hao ni baadhi tu ya stalkers waliosumbua celebrities wa  HOLLYWOOD,wapo wengi na wengine tayari walishawahi hadi kuwadhuru baadhi ya celebrities........Stay tuned for our upcoming posts..TCHAOOO..

No comments:

Powered by Blogger.