Breaking News
recent

WATU WA KAWAIDA WALIOFANANA NA MASTAR HOLLYWOOD.

Watu wanasemaga duniani wawili wawili kuna possibilty kuwa kuna mtu kafanana na wewe sehemu flani dunia hii.Leo nataka kukuthibitishia msemo huu kwani nakuletea baadhi ya watu wa kawaida tu ambao wamefanana na ma-star wa hollywood,just imagine utajisikiaje iwapo ungekuwa unafanana na mmoja wama-star maarufu duniani.Hawa watu wamelipokea hili jambo kwa utofauti,wengine wametumia kama ni opportunity ya kupata kipato,wengine wanaona tabu kufanana na ma-star kwa kuwa kila wanapooenda watu huwasumbua  na kuwafuata wakitaka kupiga nao picha au kusaini autography..Hebu tuwacheck hao watu wa kawaida tu waliofanana na celebrities wa Hollywood.
1-Konrad Annerud na Leornardo Dicaprio
 Konrad ni kijana wa kawaida tu anayefanya shughuli ya u-bartender lakini anajikuta anapata attention kubwa kwasababu kafanana na actor maarufu wa movie ya Titanic Leornard Dicaprio.Konrad anapata wakati mgumu hadi akipita mtaani watu hupiga kelele na kumwita kwa nguvu LEO LEO..
2-Ty Jones na Ed Sheeran
 Star wa nyimbo ya thinking out loud naye ana doppelganger wake,Jamaa anaitwa Ty Jones yeye tofauti na konrad,kaamua kutumia nafasi hii ya kufanana na Ed Sheeran kupata kipato,Ty huwa anaalikwa aende katika proms nyingi akiwa kama Ed Sheeran,pia Ed na Ty wamewahi kuonana mara baada ya Ed kuona picha ya Ty katika twitter na kuona jinsi walivyofanana.
3- Chelsea Murr na Angelina Jolie.
actress mtata hollywood mwanamama Angelina Jolie nae ana mtu aliyefanana nae anayejulikana kwa jina la Chelsea Marr.Chelsea anaishi SCOTLAND kafanana sana na Angelina jolie..ingawa Chelsea amefanya plastic surgery mara kadhaa kurekebisha pua na alisema anafanya hivyo kwa kuwa pua yake ni mbovu tangu akiwa mtoto kwa sababu aliumia.
4-Rose Nicholous na Taylor Swift
Rose nae kutokana na kufanana kwake na Taylor Swift huwa anaalikwa katika events kibao aende kama  Taylor pia Rose anajipatia kipato kutokana na kupiga picha akkiwa amevaa kama Taylor.Rose huwa anapata shida kitaa na ameshawahi kukimbiliwa na kundi la mashabiki wa Taylor wakimdai picha na saini yake katika vitabu vyao vya kumbu kumbu.
5-Jacky Vasques na Ariana Grande.
Jacky Vasques Kafanana na mwimbaji Ariana Grande,kajipatia umaarufu mkubwa instagram kwa kuwa huwa ana-post picha akiwa amevaa kama Ariana.
6-Harry Styles na Cecile.
Harry Styles mwimbaji wa kundi la One Direction ana mwanadada ambaye kafanana nae,Cecile ni msichana anayeishi Denmark alipata umaarufu wa ghafla pale mashabiki wa One Direction walivyom-post katika mtandao wa kijamii twitter wakimfananisha sura pamoja na nywele kuwa yupo kama Harry Styles.
7-Dani Shay na Justin Bieber.
Dani Shay ni mwanadada aliyefanana na Justin Bieber,pia Dani ana interest na music,aliwahi kushiriki mashindano ya America's got talent na alipanda stejini kuimba wimbo maarufu wa Justin Bieber Baby.
8.Claire Louise Leeson na Kim Kardashian.
 Huyu nae anafanana na Kim ila ni kwa ku-force maana alienda hadi kwa platic surgeon wake na kumuonyesha picha ya Kim na akamwambia naomba unifanye niwe kama Kim,pia alifanya operesheni ya kung'arisha meno ili yawe kama ya Kim pia alirekebisha matiti yake pia ili yawe kama ya Kim,ndoto ya Claire ni kuwa kama Kim na tayari alitumia kiasi cha euro elfu ishirini kununua cosmetics mbali mbali yote akiwa na mpango wa kufanana na Kim.
9-Fransesca Brown  na Katy Perry.
Fransesca Brown anaishi nchini England kafanana sana na Katy Perry ,Fransesca anasema anapata shida kwa kuwa watu wakimuona humfata na kumkimbilia,kuna siku alienda kwenye tamasha la music waandishi wa habari walimfata kwa wingi wakitaka kumhoji wote walijua ni Katy Perry kumbe ni Fransesca.
Katy Perry aki-selfika na shabiki aliyefanana nae aliyekutana nae katika moja ya matamasha yake ya music.
10-Hanadi Kawas na Selena Gomes

Hanadi kafanana na Selena kuliko hata Selena mwenyewe...hahaha.
11-Andele Lara na Rihanna.
Andele ni msichana wa kawaida tu aliyefanana na Rihanna na hujitahidi kumuiga hadi style ya nywele ili afanane na pop-star huyo.
12-Johana Mercado na Miley Cyrus.
Johana Mercado ni msichana tu wa kawida ambaye kafanana na Miley Cyrus ...and yeah she's nuts too...kama Miley Cyrus,Johana pia hujaribu Ku-adjust muonekano wake ili aendelee kuwa kama Miley Cyrus.Ni hao tu baadhi ya watu wa kawaida waliofanana na celebrities.
 By the way usishangae kuona picha ya Tyrese Gibson huyu jamaa kafanana na mimi mwandishi wa hii makala hahaha usibishe sasa kwani umeniona.....stay tuned for our upcoming posts....tchaooo.

No comments:

Powered by Blogger.