Breaking News
recent

BEST LOVE SONGS IN RECENT YEARS!!


Watu wanasemaga "mapenzii yana run dunia"  na ni kweli, mapenzii yupo kila sehemu maofisini, mashuleni, vyuoni, kitaa na kwingeneko, mapenzi Kwangu naona ni very complicated phenomenal..anyway kabla sijageuka Dr Phil au Oprah ngoja nirudi Kwenye topic yetu hapo juu, tangu nienze kusikiliza love songs zifuatazo ni tracks kali Zaidi kwangu:  

Bonge La nyimbo toka kwa manadada huyu, ni moja kati ya nyimbo nazozikubali kwasababu in Mashairi mazuri, ujumbe mzur wa mapenzi, pia video ya nyimbo ni kali pia, the way Selena alivyovaa ni simply outstanding!!!


Hii nyimbo Andy Grammer anajaribu kueleza Jinsi gani unaweza ukaepuka Michepuko na kudumu ndani ya ndoa au uhusiano,Andy Grammer anajaribu Kuwasihi watu waliokuwa Kwenye relationship Kuwa hata kama wameonana na mwanamke mrembo kiasi gani au mwanaume handsome wasichanganyikiwe Bali wakumbuke Kuwa Kuna mtu wamemuacha nyumbani.

     

A thousand years by Christina perri siyo nyimbo ya kubeza, Sauti ya manadada huyu inavutia masikio ya wengi , Mara ya Kwanzaa niliusikia Kwenye movie ya Twilight na nikaukubali una ujumbe Kuntu Sana, kama hujawahi kusikiliza fanya mishe ikiwezekana download Leo

Taylor Swift huwa ananifurahisha Sana ukimuudhi tu anakutungia nyimbo mpya, kashawahi Kuwazungua Katy Perry, John mayer, Kevin Jonas na wengineo, ila blank space sijui kamtungia nani ila Nahisi ni dedication kwa ex-lovers wake wote.. Anyway nyimbo ni kali, video on fleek, kila kitu was on the ryt place Bonge La nyimbo toka kwa queen of drama.  
Kundi maarufu La Acapela PENTATONIX wanasifika kwa Kafanya cover songs nzurii had zinaipita original songs, kama walivyofanya kwa OMI wimbo wa cheerleader na nyinginezo, ila walipojaribu Kafanya cover ya wimbo huu Wa Payphone Wakazingua kwa sababu original bado Ilikuwa kali kuliko cover La PENTATONIX, hivyo Adam Livine alifanikiwa Kuwafunika Vijana watata wa PENTATONIX kwa Sauti Yake amazing ukijumlisha na rap ya wiz Khalifa.
Mara ya Kwanza nyimbo hii sikuikubali Sana Baadae nikasikiliza cover ya Glee ya  nyimbo hii, nikarudia tena original, John Legend alitunga wimbo huu special dedication kwa mke wake, John aliimba toka Moyoni na kitu chohote ukikifanya toka Moyoni lazima ufanikiwe, Bonge La  nyimbo hakuna vifaa Vingi vilivyotumika Zaidi ya piano ambalo alilipiga John Legend himself.
Hii nyimbo niliusikia unapigwa Kwenye trace urban hits, nikaanza kuuelewa on the spot, Kellys Clarkson aliutendea haki wimbo huu, beat pia lilikuwa on fire, ukitaka ku-enjoy huu wimbo usikilize na ear fon zenye bass kali kama za Sony, utafurahi mwenyewe ni trak kali.
 Nahisi had Justin Timberlake anazeeka had kufa, sidhani kama atakuja kutoa trak kali kama Mirrors, video Ipo unique , nyimbo Imesimama beat kalinyonga Justin Timberland, nyimbo ina Zaidi ya Dakika saba lakini haichosh kusikiliza hata kidogo.

Hapa nilijishauri kati ya huu wimbo au one call away by Charlie Puth, Lakin nikaamua kumuweka dogo huyu, Stitches ni wimbo unaolezea maumivu ya mapenzii, Shawn katisha humu ndani had sasa ngoma hii unafanya Vizuri billboards na nimeweka on replay katika fon.

Wengi wangetegemea nimeweka Hello, lakini Someone like you, umebeba ujumbe mzur Sana, ni Wimbo unaongele kuhusu Ku-move on katika mapenzi, ujumbe ni mzur plus Sauti Matata ya mwanadada huyu ndio utafurahi Zaidi, hala adelle she is the best Kwenye game.      

Yeah Rixton ni bendi ya Vijana wannne, lakini Anayeimba ni mmoja kama anavyofanya Adam Levine katika kundi La Maroon 5, me &  my broken heart pia inazungumzia maumivu ya mapenzi, Rixton wameelezea maumivu ya kuachwa au Kukataliwa na yule umpendaye.

La da dee ndio jina La wimbo wa kijana asiye na skendo cody Simpsons, dogo anajua Sana uzuri wa nyimbo ya La da dee cjawahi kuuona hata kwa Justin Bieber, kwangu hii ndio the best love song, niliusikia katika animation ya Cloudy with a chance of meatballs 2, ulitumika kama soundtrack katika animation huyo, ni Bonge La wimbo na sidhani kama atakuja kutoa trak kali kama hii tena teh teh ila tusubiri maana cody hatabiriki.. Hii ndio list yangu bora ya love songs I hope you enjoyed, stay tuned kwa posts zifuatazo katika blog  yetu.. Tchaooo!!!    



No comments:

Powered by Blogger.