Breaking News
recent

UTATA WA NYIMBO YA "HELLO" KATI YA LIONEL RICHIE NA ADELE.




Ukiongelea traki zilizofanya vizuri mwaka Jana mwishoni,lazima utakitaja kibao cha mwanadada Adele HELLO,kibao hicho kilikimbiza chati mbali mbali na kushika namba moja Billboards.Lakini zilipopita siku chache tu tangu Adele aachie ngoma hiyo wadau wengi wa muziki walikifananisha na kibao cha HELLO cha zamani cha msanii Lionel Richie.Vibao hivyo vinafanana sana "intro" ukiangalia video inayoonyesha muunganiko wa hizo track mbili "mash up" utaona mfananano.



Lionel Richie katika interview na THE SUN aliongelea nyimbo hiyo ya Adele,Lionel Richie akasema ni kweli haurusiwi kutumia maneno ya mtu bila kumtaja "acknowledgement",alisema alifikiria kumshitaki Adele kwa kosa la kuiba intro ya nyimbo yako,Lionel Richie mwenye miaka 66 alisema alimpigia simu mwanasheria wake ili wajipange kumpeleka mahakamani Adele ila wakashindwa waanzie wapi kwasababu neno "hello" halimilikiwi na Lionel Richie.Lakini baadae    akasema kitendo hicho ni kama utani,kwani nyimbo ya Adele ni nzuri na yeye pia ni msanii mzuri.Lionel Richie pia alisema anatarajia kuwa kuna siku atafanya kolabo na Adele.

Ukitoa sakata hilo la kidaiwa kuwa ameiba nyimbo ya Lionel Richie, Adele pia alishawahi kuburuzwa mahakamani na msanii wa uturuki Ahmet Kaya alidai kuwa nyimbo ya "million years" ya adele ni yake,Ahmet alisema mashairi yaliyoimbwa humo yameigwa kutoka kwake.

No comments:

Powered by Blogger.