Breaking News
recent

COVER SONGS KALI NA MBOVU KUWAHI KUIMBWA NA PENTATONIX.

Pentatonix ni Kundi maarufu la kuimba bila beat yaani alcapella,Katika post huko nyuma niliwahi kuwapa info kidogo kuhusu hawa jamaa toka kundi lilipotoka hadi lilipo kwa sasa.Pentatonix wanasifika kwa kuimba nyimbo kutoka kwa wasanii wengine cover songs,Pentatonix wakiimba nyimbo ya mtu mara nyingi wanaipatia kwa kuwa inakuwa tamu kupita hata original lakini pia kuna mara chache wanakosea kidogo..anyway leo nakuletea baadhi ya cover songs kali pamoja na mbovu kuwahi kuimbwa na kundi huli matata.Cover Songs kali kuwahi kuimbwa na Pentatonix ni kama vile;


Little Drummer Boy,katika cover songs kundi hili la pentatonix waliutendea haki vilivyo wimbo huu.Original wimbo wa LIttle Drama Boy ni wa kidini ukiimbwa hasa na Wakatoliki kipindi cha kuhadhimisha sherehe ya x-mass.kwangu mimi ni ilikuwa first time nawasikia kundi hili na nikaupenda wimbo huu na hapo nikawa fan wao mkubwa na kudownload albam kibao.
Hadi kwa sasa wameshafanya cover songs nyingi kama Little Drummer Boy kwa aajili ya x-mass,kwangu huwa naona x-mass haijakamilika mpaka nisikie traki ya Pentatonix.
Evolution Of Beyonce,Pia Pentatonix walifanya kufuru katika traki yao waliyounganisha nyimbo kibao kutoka kwa Beyonce na wakaiita hiyo cover song Evolution Of Beyonce,Wakiwa na maana kuwa wameunganisha traki kutoka miaka ile kipindi Beyonce anatafuta jina mpaka miaka hii ambayo kawa diva wa music duniani kote.
Katika Cover Yao Pentatonix walijumlisha traki kibao kutoka kwa Queen Bee kama vile crazy in love,if i was a boy,move your body,countdown,hello,de ja vu,single ladies na nyingine kali,bonge la cover kutok kwa Pentatonix they killed it,,literally.
 Cheerleader,pia Pentatonix katika miaka ya karibuni waliachia cover ya wimbo wa cheerleader daah hii nayo ilikuwa shiiidaaaa,niliukubali sana hasa sehemu aliyoimba mitchie pia pale mwishoni sauti ya kelvin na mwanadada kristen inaweka combination adimu,Kweli Pentatonix  is the best alcapella group.
 Ni kweli Cheerleader Original kali ila Cover song ya PENTATONIX ni moto wa kuotea mbali,Original ipo slow sana tofauti na cover ambayo ipo fast and catchy.
 Hata uwe unajua kiasi gani utafanya makosa sometimes ingawa ni kwa nadra lakini Pentatonix nao kuna cover songs utaona kabisa original imeifunika na hii imewatokea katika traki chache kama vile;
Payphone,huu wimbo original aliimba Adam Levine wa kundi  la MAROON 5 akiwa pamoja na rapper machachari Wis Khalifa,pentatonix cover yao ya wimbo huu haikuwa mbaya kivile ila kwa standard yao ilikuwa ni cover ya kawaida sana Pentatonix walipoteana kabisa katika traki hii.
Hii nyimbo original yake ilikuwa perfect hivyo ikapelekea Pentatonix kutoa kitu unique ambacho ndicho wanapewa mashabiki wao kila siku,Adam Levine alinyonga hii traki cover lilikuwa meaningless tu original traki ndiyo ilikuwa kali mnoo.
Happy,Pentatonix pia hawakuitendea haki nyimbo ya pharel Williams ya happy,katika cover waliyoniboa Pentatonix hii namba moja,Pentatonix walikuwa off kabisa throughout the song tofauti na traki nyingine hii walishindwa kabisa kuitendea haki.

traki ya happy ilikuwa kali yenyewe tu kiasi kwamba hadi cover songs kama hii ya Pentatonix ikaonekana ya kawaida sanaaa.unajua sometimes imabidi ukubali nyimbo nyingine iachwe kama ilivyo ukiweka makeke tu unaiharibu..ndicho kilichowatokea Pentatonix katika traki hii ya Happy....
 angalia video inayoonyesha cover songs bora 10 kutoka kwa kundi la Pentatonix....tchaooo and stay tuned for our upcoming posts...

No comments:

Powered by Blogger.