Breaking News
recent

TOM HOLLAND ALIVYOUTENDEA HAKI UHUSIKA WA SPIDER MAN.

Tom Holland ni kijana Kutoka nchini ENGLAND,na ndiye ambaye MARVEL wameona anafaa kuuvaa uhusika wa Spider man.Ni miaka 14 sasa imepita tangu movie ya  Spider man ionekane katika ulimwengu wa cinema,na miaka hiyo yote uhusika wa Spider Man umevaliwa na watu watatu tu ambao ni Toby Miguare,Andrew Garlfried.Kabla hajaonekana katika movie ya CAPTAIN AMERIC; CIVIL WAR Tom Holland alipingwa sana na wadau wa movie wakidai hafai kuwa Spider Man Mpya na Tom kawaondoa hofu baada ya kufanya vyema katika CAPTAIN AMERICA;CIVIL WAR, Spider Man wote waliopita walipendwa mara baada ya kuvaa mask lakini Tom Holland sekunde chache tu alivyoonekana hata kabla ya kuvaa custome yake wadau tukamkubali.Nimesoma somewhere mtandaoni wameandika kuwa 'tom holland stole the scene from Robert Downey Jr[iron man]and it is not easy to steal the scene from Robert Downey jr...ikiwa na maana kuwa Tom Holland alimfunika Robert Downey Jr katika dialogue yao,ingawa waliongea kidogo Tom alionekana kuwa more interesting than Robert,kama unafuatilia movie kwa ufasaha utajua point yangu ilipo.
TOBY MIGUARE,ANDREW GARFLIED NA TOM HOLLAND.
Leo nilikuwa na ratiba tight lakini kila nilipopata nafasi nilikuwa naicheki movie ya CAPTAIN AMERICA;CIVIL WAR na kurudia scenes kadhaa hasa kutoka kwa SPIDER MAN na BLACK PANTHER nilipenda sana jinsi MARVEL walivyo-introduce wahusika..dah hawa jamaa noma..sorry DC.
 Tom Holland hakupata kiurahisi nafasi ya kuwa Spider man kuna mastar kadhaa walifanya audition lakini walishindwa na bahati ikamdondokea Tom Holland.
BAADHI YA MASTAR WALIOJARIBU KUOMBA  NAFASI YA KUUVAA UHUSIKA WA SPIDER MAN
HADI TYLER WILLIAMS NAYE ALIKUWA KATIKA ORODHA HIYO.
Tom Holland kabla hajaonekana katika CAPTAIN AMERICA;CIVIL WAR amewahi kuonekana katika movie kadhaa lakini yenye jina sana ni ile aliyekuwa na Chris Hemsworth ambaye naye anatamba na movie ya THOR wawili hao walionekana katika movie ya IN THE HEART OF THE SEA
TOM HOLLAND katika movie ya IN THE HEART OF THE SEA
Tom Holland bado sio the best spider man up to date bado kaonekana kidogo tu tutam-judge katika movie yake peke yake SPIDER MAN;HOMECOMING lakini Tom Holland Is the funniest spider man up to date Toby na Andrew wanafurahisha lakini Tom Holland ndiye aliyenikosha sana hasa jinsi alivyokuwa ana crack jokes kipindi anapigana na falcon pamoja winter soldier jamaa alikuwa so hilarious,Ant man naye hakuwa nyuma wote walitivunja mbavu sipati picha kama deadpool angekuwepo.
SPIDER MAN VS WINTER SOLDIER.
Spider man wa sasa pia yupo so strong,spider man kapigana na captain America,ant man,winter soldier na falcon wote kawatoa jasho just imagine captain Rodgers na ukongwe wake wote ule katolewa jasho na a teenager Toby na Andrew hawajawahi pambana na adui wa kutisha kivilee.
 kama nilivyoandika hapo nyuma ukweli ni kuwa Tom hollland stole the scene from Robert Downey jr,Tom alimfunika kiana Robert Downey na inahitaji kipaji cha hali ya juu kumfunika actor kama Robert katika scene moja yani ni sawa Ray wa Bongo movie apewe scene akiwa na shah rukh khan na amfunike licha ya kuwa Ray wa mchangani na SRK ni wa kimataifa.Tom Holland aliuvaa uhusika wa peter parker kwa kipaji cha hali ya juu,spider man inabidi awe social insecure [mtu mwenye aibu nyingi mbele kwa watu]-Peter Parker anavyomuona Tony Stark nyumbani kwake anamsalimia kwa aibu sana,math genius[awe ana akili sana na hesabu pia awe anajua]-Peter anamwambia Tony kuwa katoka kufanya test na kulikuwa na algebra na kafanya poa,pia hata ukicheki room lake Tony anaona devices kadhaa na Peter anamwambia i made them, spider man inabidi awe secretive hii ni kama principle kwa superheroes wote,wanaficha siri hata kwa watu wao wa karibu lengo kubwa ni kuwalinda-Peter anamwambia Tony hakuna mtu yoyote yule anayejua kuwa yeye ndiye spider man hata aunt yake aitwaye May....kwa ufupi Tom Holland ndiye Spider Man ambaye mashabiki wanastahili kupewa..asante sana kampuni ya MARVEL kwa mwendo huu kampuni ya DC COMICS wataendelea kusubiri though nasubiria kwa hamu SUICIDE SQUAD I hope DC hawataniangusha....anyway turudi kwa Tom Holland..nasubiri kwa hamu SPIDER MAN;HOME COMING itakayotoka mwakani 2017 i hope Tom Holland atatuonyesha kile alichotuonjesha katika CIVIL WAR,na kuprove theory ya mashabiki wengi kuwa marvel never miscast- ikiwa na maana kuwa kampuni ya MARVEL huwa haikiosei kuchagua actors wa kuvaa uhusika katika movies.
Stay tuned for our upcoming posts...this month ni wa CAPTAIN AMERICA;CIVIL WAR hivyo posts nyingi nitawaleta wao,endelea kuvisit na kushare link yetu....tchaoooo.

No comments:

Powered by Blogger.