Breaking News
recent

ANGALIA MAKOSA YA KWENYE MOVIES.

Aliyekuambia HOLLYWOOD hawakosei nani, hata wao ingawa ndio industry bora ya movie duniani kuna baadhi ya makosa yanatokea either katika shooting au editing..picha hapo chini ntakuonyesha baadhi ya makosa madogo na makubwa ambayo hukuyaona ila wataalamu wa Movies kwa kutumia jicho la tatu wameyagundua makosa hayo.
Katika movie ya FRIENDS,ukiangalia katika scene hii utagundua watu waliopo nyuma ya hawa wawili walibadilishana nafasi,msichana alikaa upande wa kushoto lakini mara anaonekana yupo upande wa kulia katika scene hiyo hiyo moja.
Katika movie ya SPIDER MAN scene inamuonyesha Peter akirusha utandu na kuivuta taa na ikavunjika,lakini cha ajabu scene ya pili taa ipo pale pale na wala haijaharibika wala kuvunjwa.
katika movie ya HARRY PORTER mmoja wa member wa Camera crew anaonekana katika scene mojawapo,inaelekea katika kuedit walisahau na camera man akaonekana katika movie.
katika movie ya TWILIGHT tattoo ya Jacob kipindi anaongea na Belle inaonekana ipo juu ya bega,lakini katika scene nyingine akiwa anaongea na Edward tattoo inaonekana ipo chini.
Katika movie ya TERMINATOR 2 Arnold anafyatua risasi kichwa cha terminator lakini cha ajabu ni kuwa,kichwa kinapasuka kabla hata risasi haijafyatuiliwa.

















katika movie ya TERMINATOR 3 scene moja inaonyesha plate number ya ndege tofauti na nyingine,ndege ilipokuwa chini na pale ilipokuwa angani plate number ni tofauti na ndege ni moja.
Katika movie ya X-MEN 2,Raisi katika scene anaonekana akiwa na file jeupe lakini sekunde kadhaa mbele anaonekana akiwa na file la blue wakati mikono yake haikwenda popote.
Katika movie ya LORD OF THE RINGS Frodo jeraha lake linabadili nafasi,katika scene moja lilikuwa upande wa kushoto lakini katika scene nyingine jeraha lile linaonekana lipo upande wa kulia.
Katika movie ya TERMINATOR 3 scene moja inaonyesha gari lina kioo cha mbele lakini sekunde kadhaa mbele gari lile lile linaonekana lakini likiwa halina kioo.
Katika movie ya TITANIC ukiangalia kwa umakini utagundua kuwa katika scene hii Rose aliugonga mkono wa Jack na shoka lakini walitudanganya kuwa hapa Rose aligonga pingu iliyomfunga Jack.
katika movie ya CASINO ROYALE scene inamuonyesha James Bond akim-kiss msichana huku akiwa na mchanga mgongoni kwakw,lakini katika scene hiyo hiyo mchanga wa mgongoni hauonekani tena mgongo unaonekana msafi tu.
Katika movie ya THE BOURNE IDENTITY katika scene mojawapo Bourne anam-kiss msichana huku mkononi akiwa kavaa saa upande wa kulia lakini baadae kidogo katika scene hiyo hoyo saa inaonekana imehamia upande wa kushoto.
katika movie ya THE MATRIX katika scene mojawapo Agent Smith anafanya mahojiano na Neo,Neo anaonekana yupo kwenye kona ya chumba,lakini cha ajabu reflection ya Neo katika miwani ya Agent Smith inaonyesha kuwa Neo kakaa kwenye kiti.
Hayo ni baadhi tu ya makosa katika movies mbali mbali,angalia pia na hiyo video ujionee makosa mbali mbali katika movies mbali mbali maarufu Hollywood.Tchaaaoo.....Stay tuned for our upcoming posts.

No comments:

Powered by Blogger.