kabla sijaiangalia movie ya X-MEN APOCALYPSE nilikuwa nina shauku sana ya kumuona Quick Silver,huyu jamaa ni superhero anayesifika kwa kuwa na kasi sana,speed yake haina tofauti sana na the flash ingawa flash anasema he is the fastest man alive.Kabla hujacheki X-MEN APOCALYPSE unakumbuka mambo aliyoyafanya Quick Silver katika X-MEN DAYS OF FUTURE PAST, ile scene anawasaidia Wolverine na Professor Xavier kumtoa Magneto Jela, ni moja ya scene bora kabisa kuwahi kufanywa katika ulimwengu wa movie. Quick Silver alikuwa yupo fast sana kiasi kwamba vitu vingine vinaonekana kama kwenye slow motion.
Ni bonge moja la scene ni kitendo kilichochukua dakika mbili kwa sisi viewers lakini makers wa movie walitumia wiki kadhaa kufanya scene hiyo mpaka ikaonekana kuwa kali vile.
Quick Silver katika ubora wake
Quick silver akifanya yake
Quick silver akiwapa shida maadui.
anyway ile scene ya kwenye days of future past ilikuwa chamtoto ,Quick Silver alikuja kufunika kwenye apocalypse,tuliona jinsi alipofoka katika shule ya Profesa Xavier na kukuta kuna mlipuko, kwa jinsi alivyo na kasi anawaokoa watu wote ndani ya dakika 3 tu.
Quick Silver akiokoa watu katika moto.
Quick Silver akiwasili nyumbani kwa profesa na kukuta kuna mlipuko.
Je unajua hii scene waliifanyeje...Ngoja nikupe mwanga kidogo uelewe jinsi walivyofanya mpango wote katika shooting.
Walitumia camera aina ya phantom ambayo huchukua picha kwa haraka sana,camera hii ina-shoot frames 3000 kwa sekunde,hivyo kwa kutumia hii camera ikasidia sana kufanya scene ionekane ya haraka sana kupitia Quick Silver.
Camera ya phantom ikifanya yake.
Pia katika kufanya scene hii walifunga nguo kubwa kama blanket hivi ambalo lilisaidia kuwadaka watu waliokuwa wanaokolewa na kurushwa na Quick Silver.
Jinsi watu walivoweka katika kufanya scene ya Quick Silver
Quick Silver akifanya mambo yake.
Blanket kubwa lililowekwa katika kufanya scene ya Quick Silver.
Evan Peters jamaa ambaye kauvaa uhusika wa Quick Silver
Director wa movie ya X-MEN APOCALYPSE bwana Brayn Singers alisema scene hiyo ndogo tu ya dakika tatu ilitumia wiki saba mpaka kukamilika, anasema kutoka na scene hiyo Evan ndiye actor aliyeshinda sana location kuliko actor mwingine yoyote yule wa movie hiyo
Ukiangalia video hiyo ndiyo wameonyesha details sana ila kwa ufupi hivyo ndivyo Quick Silver alivyofanikiwa kutushika na scene yaka matata sana katika movie ya X-MEN APOCALYPSE.
Kwa scene ile kali nahisi Quick Silver kwa kwenye X-MEN yupo fast sana kuliko hata Quick Silver wa kwenye AVENGERS,pia kuliko hata The fash......well it is just my opinion.
Stay tuned for our upcoming posts ,follow us on insta @feel-design-96 and also like our facebook page FeelDESIGN......
ANGALIA JINSI SCENE YA ''QUICK SILVER'' KATIKA MOVIE YA'' X-MEN APOCALYPSE'' ILIVYOTENGENEZWA.
Reviewed by Unknown
on
12:08
Rating: 5
No comments: