Breaking News
recent

UTATA KUHUSU NYIMBO MPYA YA KATY PERRY.

Ni siku tatu tu toka mwanadada katy Perry aachie ngoma yake mpya iitwayo RISE, Nyimbo yake hiyo mpya itatumika kama theme song ya mashindano ya OLYMPICS 2016 yatakayofanyika jijini RIO DE JANIERO nchini BRASIL.Katty Perry alikuwa hajatoa nyimbo yoyote ile tangu October mwaka 2013 hivyo ujio wa ngoma yake mpya umechukuliwa kitofauti kidogo.Ukiisikia nyimbo ya RISE ina mashairi ya kuhamasisha na si ajabu kwa nyimbo hiyo kutumika katika OLYMPICS kwa sababu inakidhi mahadhi ya ki-athelete .Nyimbo mbili moja hii RISE na nyingine MAKE ME ya Britney Spears ndio theme songs katika mashindano ya OLYMPICS mwaka huu.
 
Nyimbo ya MAKE ME ya Britney Spears pamoja na nyimbo ya RISE ya Katy Perry.
Licha ya kuwa  nyimbo ya RISE inaonekana kabisa ni kwa aajili ya mashindano ya OLYMPICS lakini inaonekana pia nyimbo hii ina maana pana kuliko inavyoonekana.Nyimbo hii ya RISE inasemekana ikawa inamhusu Taylor Swift [Huko nyuma nishawahi andika kuhusu beef lao], Nyimbo ya RISE inaonekana kama Katy Perry kaamua kumjibu Taylor siwft ambaye aliaachia kibao cha BAD BLOOD akimponda Katy Perry kuwa ni msaliti na ndiye aliyesababisha urafiki  wao uharibike,ukiusikia wimbo huu na kutafakari lyrics utagundua kuna ujumbe fulani.

 Beef la Taylor na Katy  ni la muda mrefu sasa, na katika wote wawili sijaona jitihada kama wanataka kuurudisha urafiki wao au na kuna vijembe vinaendelea chini chini hasa katika mitandao ya kijamii kama snap chat na instagram wakipondana kimafumbo.Ila utata unarudi pale pale, ni kweli kuwa hii nyimbo inamhusu Taylor au ni theories tu kutoka kwa fans, kama Katy angekuwa na nia ya kujibu blood blood angefanya hivyo mapema sana, lakini kwanini kajibu wakati huu wakati ni muda mrefu sasa umepita tangu apewe dis katika nyimbo ya bad blood.
Taylor Swift na Katy Perry pindi ewalipokuwa marafiki.


katy Perry aliongea haya kuhusu ngoma yake hiyo mpya ikiwa tayari ina viewers milioni 10 ndani ya siku 3 tu...''hii nyimbo nilikuwa nataka niitoe kwa miaka mingi sasa ilikuwa ndani ya kichwa changu na hatimaye nimeshaitoa, nimeamua kuitoa sasa na sikutaka kusubiri mpaka nitoe album mpya,kwa sababu sasakuna umuhimu wa watu ulimwenguni kuungana, kwa sababu pamoja tunafanikisha na kuibuka washindi dhidi ya uoga ndio maana nimeufananisha wimbo huu na washiriki wa OLYMPICS wanaoenda kushindanakwa nguvu na bila uoga, na kutukumbusha kuwa kwa pamoja tutafanikisha.Natumaini nyimbo hii itawahamasisha kushirikiana na kuinuka kwa pamoja.Nawashukuru sana NBC kwa kuamua kuuchagua wimbo huu utumike katika mashindano ya OLYMPICS'' hayo ni maneno ya Katy Perry kuhusu nyimbo yake ya RISE.

Baadhi ya LYRICS katika nyimbo ya  RISE .
video wa nyimbo hii ni hiyo hapo juu........Stay tuned for our upcoming posts....tchaooo

No comments:

Powered by Blogger.