Breaking News
recent

KWANINI SHAH RUKH KHAN HAITAKI HOLLYWOOD.

Marekani ndio nchi inayosifika kwa ku-make movies kali duniani kote,na ni ndoto ya actors wengi kufanya movies marekani maarufu kama hollywood. Actors wengi kutoka pande mbali mbali ulimwengu kote huona kama hollywood ni kikomo cha mafanikio, lakini hali ni tofauti kidogo kwa Shah Rukh Khan maarufu kama the badshah of bollywood,ambaye yeye licha ya kuwa actor maarufu sana India hajawahi fanya movie hollywood.kwa sasa actors kutoka India wameona kama fashion kwenda Hollywood lakini SRK katulia tu
Deepika Padukone na Priyanka Chopra ni kati ya majina makubwa toka Bollywood ambao wana projects Hollywood.
SRK alipohojiwa na indian times aliwaambia mambo yafuatayo kuhusu kwanin hadi sasa hajafanya project yoyote ile hollywood wakati wengine kama Deepika na Priyanka wameonyesha nia na kuchangamkia fursa.
SRK na Kajol katika movie ya DILWALE
 SRK alisema yeye hajakidhi viwango vya kufanya movie hollywood,Srk aliwaambia Indian Times kuwa anahisi hana kipaji cha kutosha cha kufanya movie huko, seriously hahaha..hapa SRK alituongopea eti hajakidhi viwango, hadi Anil Kapoor tayari kaonekana movie ya hollywood, sasa kama hadi Anil Kaapoor aliyeonekana katika movie ya MISSION IMPOSSIBLE-GHOST PROTOCAL kashafanya movie Hollywood SRK atashindwaje....hao akina Priyanka na Deepika ameshawahi kufanya nao movies sasa kama wao wamekidhi viwango SRK inakuwaje hajakidhi.
SRK na Kajol katika premiere ya DILWALE.
Srk aliwaambia indian times kuwa yeye ana aibu sana hivyo itakuwa ngumu kwake kufanya movie hollywood,kama unavyofahamu kuwa hollywood katika movies ikiwa scene kwa mfano ya love making uhalisia inabidi uwepo na sometimes huwa wanafanya kweli,tofauti na wahindi ambao love scenes kwao ni casual kabisa.Sasa SRK yeye akijitahidi sana kashika kiuno cha Kajol au kam-kiss katrina kaif katika paji la uso,hivyo itamwia vigumu hollywood akiambiwa hata am-french kiss Angelina Jolie au Sandra Bullock.
SRK alisema kuwa yeye ana aibu sana na huwa anapata wakati mgumu kufanya project na watu wageni.
SRK alisema anaipenda nchi yake hivyo hana haja ya kwenda hollywood kuthibitisha kipaji chake, Srk aliwaambia indian times kuwa anapenda kufanya movies India na kujulikana kimataifa sio mpaka aende hollywood pekee ndio afanikishe hilo hata India anafanikisha,pia SRK alisema ana mpango wa kufanya movie moja kali sana itakayoweka historia India na duniani, lakini katika movie hiyo yeye hatakuwa actor lakini atahusika katika kuiandaa.
SRK alisema hajawahi pata ofa yoyote ile ya kufanya project ya movie hollywood,Srk anasema kuwa hajapata ofa..huu ni uongo...ni sawa na Messi aseme haondoki Barcelona kwa sababu hajawahi pata ofa kutoka klabu nyingine,wakati watu tunajua kiwango chake,Inasemekana SRK ameshakataa ofa kibao kutoka Hollywood ikiwemo ya mwaka 2013 ya kufanya project na actor wa TITANIC Leonardo Dicaprio.Pia SRK alimkatalia Jackie Chan kufanya nae movie.Hivyo kusema hajapata ofa ni kutupiga changa la macho laivu laivu.
Shah Rukh Khan na Leo Dicaprio.









SRK na Jet li [hawakuwa na nia ya kufanya movie bali walikutana tu]

Kwa mimi naona it is ok tu hata SRK asipofanya movie hollywood kwa sababu ameshajijengea msingi imara bollywood,pia SRK ni tajiri kuliko hata actors wa hollywood,mnamo mwaka 2014 SRK alikuwa analipwa fedha nyingi kuliko hadi Tom Cruise na John Depp ambao wote wana majina hollywood.SRK ana kila kitu cha kumfanya afanye project ya movie hollywood lakini kwa sasa ameamua atulie bollywood muda muafaka wa yeye kufanya movie hollywood ukifika,basi atafanya hivyo...
One day YES...Ili cover ni fan-made,ipo siku SRK atafanya movie HOLLYWOOD
stay tuned for our upcoming posts...tchaoooo

No comments:

Powered by Blogger.