Breaking News
recent

MAMBO AMBAYO UTAKE USITAKE UTAYAONA TU KATIKA KOREAN SERIES.

Mwaka 2010 niliangalia series ya Kikorea for the first time series hiyo iliyopata umaarufu kipindi kile na hadi wakati huu, ni series ya JUMONG,niliipenda lakini sio kivileee..niliangalia nyingine kadhaa ikiwemo series ya IRIS ambayo ilifanya poa na hadi lead actor wake alipata nafasi ya kwenda HOLLYWOOD na akaonekana katika movies mbili..G.I JOE na RED 2,nilikuwa tayari addicted na series kutoka U.S hivyo sikupata muda sana wa kuwafuatilia wakorea.Hivi karibuni nikawa nimerudi rasmi katika ulimwengu wa series kutoka korea maarufu kama K-DRAMA,Nikiwa tayari nimecheki series kadhaa kama vile THE CUNNING SINGLE LADY,GU FAMILY BOOK,EAST OF EDEN na nyingine nyingi ingawa niliyoipenda sana ni MY GIRLFRIEND IS A GUMIHO Series hii naipa alama 100 kwa kuwa the series gives you what you expect and more than you expect ni bonge la series kulikuwa kuna chemistry ya kuvutia kati ya characters.

Baada ya kucheck series mbali mbali kutoka Korea ,nimegundua mambo cliches au mambo ambayo yapo karibia kila series ya kikorea,mambo hayo ni haya hapa chini;
Love at first sight,yaani katika K-DRAMA ''love at first sight'' hutokea mara nyingi sana hasa katika modern k-drama ingawa katika classic k-drama sio common sana.Utakuta tu msichana na mvulana wamekutana katika lifti,au mmoja kamgonga mwingine na gari au wamegongana barabarani, yani kokote kule wanapokutana kila mmoja humpenda mwingine papo kwa papo.
Love at first sight katika K-DRAMA

Love at first sight katika K-DRAMA.
Dramatic rain scenes,Wakorea wanapenda mvua aiseeh yani ukicheki wakorea utakutana tu na scenes mvua inanyeesha ,afu utakuta mtu analia au wana-kiss ,pia mvua hutumika katika breaks ups na heart breaks utakuta jamaa baaada ya kuwa dumped au msichana baada ya kumfumania boyfriend wake anakimbia nje kulia huku mvua inanyesha.

heart-break scene
Misiba mingi katika Korean series huambatana na mvua.
Wakorea wanapenda kubebana,huu sasa umekuwa kama ugonjwa katika K-DRAMA yaani JIPU kabisa ,hii tabia ya kubebana ni common katika modern na classic K-DRAMA,katika scenes kadhaa watabebana tu ikiwa njia mojawapo ya kuonyeshana upendo.
Baadhi ya K-DRAMA ambapo wahusika wakuu  wamebebana.
Wakorea katika K-DRAMA wakiwa wamebebaba kama kawaida yao.
Busu la mwendo kasi ''suprise or awkward kiss'',Hapa inatokeaga katika K-DRAMA utakuta a boy and a girl wana-kiss ghafla tu au katika maeneo ambayo hawakutegemea na inatokea bahati mbaya tu.Kwa mfano sometimes utakuta ni marafiki tu ambao kila mmoja ana feelings kwa mwengine lakini hawajaambiana hivyo inapotekea chance wanajikuta wana-kiss tu.
Mfano wa Busu la mwendo kasi katika K-DRAMA.
Busu la ghafla au mwendo kasi katika K-DRAMA.
Love Triangles,hii sasa ndio too much katika K-DRAMA ,Love Triangles inatokea kwa mfano marafiki wawili wanakuwa wanampenda msichana mmoja na yule msichana mmoja anawapenda wote wawili au mmoja kati yao.
Love triangle katika K-DRAMA.
Love triangle nyingine katika K-DRAMAS.
Asubuhi wanaamka wasafi ukafikiri usiku hawakulala,hii katika series kadhaa hasa modern K-DRAMA utakuta mdada katoka kuamka hata mswaki hajapiga ila yupo full na make up juu.
Wakorea pia huwa wananiboaga hapa.....1-HAWAKUI [yaani utakuta unaangalia series wanaandika after 20 years unakuta mtu yupo vile vile hata hajabadilika]....2-WANAPENDA KUJIUA [yani wakorea kama  wahehe hivi mdada akibakwa tu anakimbilia kujiua wapo so suicidal]....Hayo ni baadhi tu ya mambo ambayo utayakuta katika K-DRAMA nyingi...Tchaoo stay tuned for our upcoming posts.

No comments:

Powered by Blogger.