Breaking News
recent

MANENO NA MATENDO YANAYOJIRUDIA KATIKA MOVIES NYINGI HOLLYWOOD.

Unaposikia neno HOLLYWOOD mara moja katika kichwa chako utafikiria kuhusu movies,wala hutafikiria maeneo ya kuvutia ya los Angeles,California ambapo ndipo HOLLYWOOD ipo,wala hutafikiria kuhusu majengo ya kuvutia yaliyopo jimbo la california,utafikiri kuhusu movies tu..Naam hata mimi nataka nikupeleke huko huko ,sina mpango wa kuongelea geography ya HOLLYWOOD bali nataka kuongelea kuhusu mambo yanayofanyika ndani ya HOLLYWOOD na hakuna jipya HOLLYWOOD ni movies tu.Ukiwa unacheck sana movies unajikuta unahisi ukatabiri baadhi ya movies mwisho wake utakuwaje,au ukicheck movie flani utaona kama inajirudia au utahisi kitendo kilichotendeka katika ile movie ushawahi kukiona katika  movie nyingine,sometimes unakumbuka au haukumbuki ni katika movie gani lakini unakuwa na ile idea kuwa hili neno au hiki kitendo kishawahi fanyika katika movies nyingine.Aina hii ya hisia  inaitwa de ja vu,yani ni pale unapokutana na kitu na ukahisi kinajirudia au ushawahi kuki-experience hapo kabla.Kwa mimi de ja vu katika movies imekuwa hali ya kawaida kwa sababu nacheck movies nyingi.Hapo chini nakuletea baadhi ya maneno na vitendo yaliyojirudia katika movies nyingi HOLLYWOOD na sio HOLLYWOOD pekee hata katika movie industries kutoka nchi mbali mbali.
1.Dont you die on me..

Hili neno limekuwa common sana katika movies,hutumika hasa pale mtu anapokuwa anakaribia kufa yupo kifuani kwa mtu maybe ni rafiki,mke,mume,mtoto,baba au mama yake,kwa mfano katika vita mmoja wa wanajeshi akipigwa risasi mwingine humuondoa katika battle field na kujaribu kumtibu huku akimwambia maneno please DONT YOU DIE ON ME..Hii imetokea katika movies kama vile FACE OFF,LORD OF THE RINGS na nyingine nyingi .
2.GET OUTTA THERE na SHIT'S ABOUT TO GO DOWN.
Haya pia ni maneno ya kawaida sana kutumika katika movies, yote hutumika kuwaonya watu waondoke mahala fulani kwa kuwa kuna hatari itatokea kwa mfano mlipuko wa bomu,maneno haya yametumika katika movies kama vile LORD OF THE RINGS,ALIEN,THE MATRIX na AVATAR.
3.A STORM IS COMING
 
Haya maneno pia hutumika kuonya juu ya hatari inayotarajiwa kuja mbeleni,baadhi ya movies ambapo maneno haya yamesikika ni NIGHT AT THE MUSEUM,THE DARK KNIGHT RISES na HARRY PORTER AND THE ORDER OF PHOENIX,kama inavyoonekana katika picha hapo juu pamoja na scenes kutoka katika movies.
4.YEAH YOU BETTER RUN
Haya maneno yametumika katika movies kama vile RANGO,WILLOW na BAT MAN BEGINS,katika matukio mbali mbali hasa pale adui anamuachia kidogo mtu akimbie akiwa na nia ya kumfata kwa nyuma.

5.NOOOOOOOOOOO.....
 Dah limetumika movies nyingi sana tena sana,nahisi karibia kila movie ya action,hasa pale staring anopokuwa amefeli jambo flani.
Hayo juu ni MANENO tu tukihamia katika vitendo vilivyojirudia sana katika movies ni kama vifuatavyo;
1.Kitendo cha PAKA kutokea na kumuangalia mtu usoni afu kuendelea na safari yake.

hiki kitendo kinatokea sana katika movies yenye kutisha kama ilivyoonekana katika baadhi ya movies kama vile SCREAM,THE AMITYVILLE HORROR,FRIDAY THE 13TH na THE GREAM RIPPER.Paka huonekana na kumwangalia mtu usoni hii yote ni kwa nia ya kuwaogopesha watu wanaoangalia au kuuonyesha tension katika movie ya kutisha.
2.Kitendo cha Wamerekani wengi kukimbilia MEXICO.

Hiki kitendo kipo movies kibao ,mara nyingi wahalifu kutoka marekani hukimbilia nchini MEXICO kwa nia ya kujificha.Hii ishatokea katika movies kama vile LOVE AND a.45,THELMA AND LOUISE,FROM DUSK TILL DAWN,THE LAST STAND,THE CHASE,THE GATE AWAY,BLUE STREAK,TOUGH GUYS na THE SHAWSHANK REDEMPTION.
3.Kitendo cha mtu kuota anam-kiss msichana akiamka anakuta alikuwa analambwa na mnyama.
Hiki kitendo ni common sana katika movies ..utaona jamaa amelala analala anahisi anambusu msichana kumbe ni mnyama anamlamba lamba ili jamaa aamke,hiki kitendo kimetokea katika movies kadhaa kama vile SHANGHAI NOON na hata katika series ya GAME OF THRONES.
4.Sex ya MWENDO KASI.
 Katika movies nyingi MAREKANI,wahusika hukutana katika scene flani scene inayofuatia tayari wameshalala pamoja kama inavyoonekana hapo juu ilitokea katika STUCK ON YOU,HOMELAND,DIE ANOTHER DAY na KNOCKED UP.
5.Music ndani ya Lifti
Hiki kitendo cha watu kuwa katika Lifti alafu simu ya mtu ikaita huku ikiwa na mlio wa ajabu,au katika scene ya Lifti utasikia music unasikika kuashiria tukio linalotarajiwa kufanyika na wahusika wa movie flani,kama tulivyoona katika WALL-E,DAWN OF THE DEAD,SPIDERR-MAN,TEENAGE MUTANT NINJA,MR. AND MRS. SMITH na X-MEN ORIGONS;WOLVERINE.
 Hayo ni baadhi ya maneno na vitendo ambavyo kwa namna moja au nyingine hujirudia sana katika movie HOLLYWOOD....Tchaaoooo...Stay tuned for our upcomong posts....

No comments:

Powered by Blogger.