FACEBOOK KUONGEZA BUTTON YA "DISLIKE".
CEO wa Kampuni Ya mtandao wa kijamii FACEBOOK bwana Mark Zuckerburg ametangaza kuwa FACEBOOK ina mpango wa kuongeza button ya "dislike".Mark alisema watumiaji wa mtandao huo walikuwa wanaomba button hiyo iongezwe kwa muda mrefu sasa tangu button ya "like" iwekwe mwaka 2009.Mark alisema nia ya kuweka button hiyo ni kuwawezesha watumiaji wa-dislike picha ambazo hawajapendezwa nao au pia iyo button itakuwa kama "sorrybutton" kwamba mtu akiweka post kuhusu taarifa ya kusikitisha kama msiba au ajali na majanga mengine mtu anaweza aka-dislike kwa sababu ni taarifa za kusikitisha na sio kuweka button ya "like" kama ilivyozoeleka.Hadi sasa FACEBOOK hawajasema hiyo "dislike" button itakuwaje ila wengi wanahisi itakuwa "thumbdown" (dole gumba chini) kwa sababu button ya "like" ni "thumbup" (dole gumba juu).
No comments: