Breaking News
recent

JE TUPAC YUPO HAI?

Polisi mstaafu mmoja aliyejulikana kwa jina la David Myers alitoa taarifa za kushitukiza jana nchini marekani baada ya kudai kuwa rapa mahiri wa zamani Tupac omar Shakur aliyefariki miaka 20 iliyopita kuwa yupo hai.2pac alifariki mwaka 1996 baada ya kupigwa risasi akiwa ndani ya gari maeneo ya las vegas Nevada nchini Marekani. 2pac alifariki siku sita baadae mara baada ya kupigwa risasi.Habari iliyotolewa na mtandao wa MIRROR inasema kuwa Askari huyo alisema hayo akiwa hoi kitandani.David alisema alipewa kiasi cha dola za kimarekani milioni 1.5 kusaidia ku-fake kifo cha Tupac.David anaendelea kwa kusema aliyesaidia ku-fake kifo cha 2pac hayupo peke yake wapo wati zaidi ya 30 kwa madai yake anasema kuwa mwili uliozikwa ni wa mtu mwingine na uliibwa mochwar kwa aajili ya kufanikisha zoezi hilo.David Myers alisema ameamua kuiambia duni ukweli kwa sababu anaona aibu na anakaribia kufa hivyo angependa afe kwa amani.Je david Myers anasema ukweli? Au ni wale wanaotafuta umaarufu kilazima? Kweli 2pac yupo hai? Na kama kweli yupo hai kwanini aamue ku-fake kifo? Is tupac or makaveli alive? TUSUBIRI.


No comments:

Powered by Blogger.