Breaking News
recent

KWANINI BAADHI YA TV SHOWS ZINAKUWA CANCELLED?

 

Huwa ni kitendo kinachowauma sana watazamaji pale unapofuatilia tv series flani alafu inakatishwa kabla haijamalizika. Tabia ya kukatisha series imefanywa na makampuni mengi makubwa kama NBC' BBC' SKYF na CW.Tv shows nyingi maarufu kama CHUCK' MISSING' ANTLANTIS' KYLE XY na nyingine nyingi zilikumbana na majanga haya.Tv shows nyingi zinakatishwa kwa sababu zifuatazo:                                        

1-Kupungua kwa chati ya watazamaji (low rating views):Kurusha episode moja katika  televisheni ni gharama sana hivyo show isipokuwa na watazamaji wa kutosha inakatishwa kwa mfano shows kama MISSING' STAR CROSSED' CULT na nyinginezo zilikatishwa kwa sababu hii.         

 2-Kukosa pesa za kutosha za kuiendeleza tv show (lack of fund for further production): Hapa watazamaji wanaweza wakawa wanatosha lakini bado faida haiji ya kutosha ya kufanya tv series iendelee.            

3-Sababu maalumu (special case) Hapa production crew wanaweza wakawa wana pesa za kutosha na watazamaji wa kuridhisha lakini show inaweza ikakatishwa kwa mfano mmoja wa wahusika muhimu wa show anakufa na inakuwa ngumu kupata mbadala basi show hiyo inakatishwa.Lakini kama series bado ipo season za mwanzo mbadala anatafutwa kwa mfano alipofariki muhusika mkuu  SPARTACUS series iliendelea kwa maana mbadala alipatikana.   

4-Sababu za kisheria (legal reasons):Wakati mwingine tv shows zinakuwa cancelled kwa sababu ni amri ya serikali kwa mfano kuna tetesi zinasemwa (bado haijathibitishwa) kuwa series ya TRAVELLER ilikatishwa kwa sababu ilikuwa inafichua baadhi ya siri za kiserikali ndio maana ikakatishwa.                   

Hizo ndio sababu kubwa za kukatisha tv shows lakini tv shows hizo mara nyingine huweza kurudishwa kwa mfano JERICHO ilikatishwa lakini ikarudishwa baada ya watazamaji kujitolea kuirudisha.Pia series ya DR WHO ilikatishwa mwaka 1989 ikaja kurudishwa mwaka 2005.Kwa upande wa Japan shows hata ziwe mbaya kiasi gani haziwi cancelled.Wanachofanya nchini japan kila show inapewa nafasi ya kurushwa hewani kwa episodes kama 13 hivi kama show ikifanya vibaya Production crew inapewa nafasi ya kuongeza episodes moja  mbili ili kufupisha tv series mpaka pale ilipotakiwa kuwa mwisho na kumalizia stori iliyobaki katika episodes hizo ili wasiwaboe tu watazamaji kwa kukatisha show kati kati.

No comments:

Powered by Blogger.