Movie Nyingi zinazofanya vizuri sokoni ni zimetoka katika nchi mbili Marekani na India.Hollywood na bollywood movies zao zina mashabiki wengi sana na pia kuna muda huwa wanaigana hasa hasa Bollywood huwa wana copy kutoka Hollywood.Hollywood na Bollywood wanatofautiana kupitia mambo yafuatayo:
1-Mahali:Hollywood haitumiki tu kama jina la kutambulisha filamu za kimarekani lakini pia Hollywood ni sehemu ambayo ipo Marekani maeneo ya Los Angeles' California.Bollywood hakuna sehemu inayoitwa hivyo ila inatumika tu kuwakilisha filamu za kihindi na Bollywood ni muungaaniko wa maneno mawili "Bombay-Hollywood" Bombay/Mumbai ni mji mkuu India na movie ya kwanza iliigizwa huko.
2-Mwanzo:Movie ya kwanza ilianza Hollywood miaka ya 1870's lakini movie ya kwanza Bollywood ilitoka mwazoni mwa miaka 1900's
3-Movie Za Gharama:Kwa upande wa Hollywood movie iliyotumia Gharama nyingi ni movie ya PIRATES OF CARIBEAN (2007) na kwa upande wa Bollywood movie iliyotumia gharama kubwa ni RA-ONE (2011).
4-Movie Zilizoongoza kwa mauzo:Kwa upande wa Hollywood movie iliyoongoza kwa mauzo ni AVATAR (2010) na kwa upande wa Bollywood movie iliyouxa sana ni 3 IDIOTS (2009).AVATAR iliingiza zaidi ya dola za kimarekani bilioni 2 wakati 3 IDIOTS iliingiza zaidi ya dola za kimarekani milioni 700.
5-Maudhui ya Movie:kwa upande wa Bollywood huwa wanachanganya maudhui mengi katika movie moja unaweza ukakuta movie ina mchanganyiko wa Action' Thriller' comedy na drama katika movie moja ila Hollywood mara nyingi wanatoa movie zinazojitegemea kimaudhui.Movie nyingi zinajitegemea kimaudhui kama ni drama basi drama tu kama ni thriller vivyo hivyo.
6-Utamaduni wa movie:kwa kawaida movie nyingi za Bollywood ni ndefu mara nyingi huwa na masaa mawili hadi matatu lakini Hollywood movie zao sio ndefu sana kuna movie hadi za saa moja.Pia Bollywood karibia asilimia 90 za movie zina nyimbo ndani yake Wakati Hollywood hawana nyimbo katika movie zao za kawaida kama movie ya muziki wanaitoa kivyake kama vile LET IT SHINE' CAMP ROCK na HIGH SCHOOL MUSICAL. 
HOLLYWOOD VS BOLLYWOOD
Reviewed by
Unknown
on
01:05
Rating:
5
No comments: