Breaking News
recent

MJUE WALTER O'BRIEN,MTU WA NNE KWA IQ KUBWA DUNIANI.

Kama unafuatilia series ya SCORPION unaweza ukafikiri series hii ni stori tu za kawaida zinazotungwa kama stori nyingine lakini hii ipo tofauti kidogo,unapoangalia series ya Scorpion inayohusu Ma-Genious kila episode inaanza na maneno haya "inspired by the life of Walter O'Brien" series hii inahusu kundi ka watu wenye akili nyingi 'Genious' mmoja wao ni "human calculato" anajua sana hesabu,mwingine ni "mechanic" aajua kutengeneza vitu mbali mbali kama magari na mwingine ni kama "behaviourilist" anajua kusoma tabia na saikolojia ya mtu,Kwa pamoja wanatatua matatizo na uhalifu mbali mbali wa teknolojia....

Tukirudi katika maisha ya kawaida Walter O'brien yupo na ni kweli ana IQ ya 197, Walter ndiye Producer mkuu wa show hii.Walter O'Brien alizaliwa Ireland mwaka 1975 alipokuwa na miaka 13 alinunuliwa Computer na wazazi wake ndipo akaanza udadisi na akafanikiwa ku-hack katika satelite mojawapo iliyokuwa chini ya NASA.Walter alifuatwa hadi nyumbani kwake na maafisa ea NASA lakini hakuelezea kwa kina nini kilifuata ila tujue tu kuna makubaliano aliuoweka na NASA ambao hadi leo unafuatwa. Walter alishinda mashindano ya kutumia computer kwa haraka nchini Ireland.Pia alipokuwa ana umri wa miaka 18 alishiriki mashindano ya olympic programing na akasika nafasi ya kidunia' kwa sasa  Walter ni CEO wa SCORPION nchini Marekani

No comments:

Powered by Blogger.