Breaking News
recent

SERIES YA EMPIRE NI BARAKA AU MAJANGA KWA WATU WEUSI?

Unapoongelea Series zinazofanya vizuri kwa kuwa na viewers wengi huwezi ukaisahau EMPIRE,Tangu episode ya kwanza inatoka hadi leo hii EMPIRE bado inafanya vizuri.EMPIRE ni series ya watu weusi Producers wake wakubwa Lee Daniels na Timbaland ni watu weusi,Wahusika wakuu aisilimia nyingi ni watu weusi (Taraji,Terrernce,Jussie etc). 

EMPIRE imeleta mapinduzi baada ya kuzipita show nyingi za kimarekani kwa kuwa na watazamaji wengi,EMPIRE ipo chini ya kampuni ya FOX.EMPIRE ikiwa chini ya watu weusi imewashitua wamerekani wenye shows kali kama THE FLASH,GLEE,C.S.I,THE ORIGINALS na nyingine nyingi.

EMPIRE inazikimbiza pia series kali nyingine za weusi kama POWER na SINGLE LADIES,lakini swali la kujiuliza je hii show imewapa manufaa watu weusi? Show hii inaonyesha jinsi maisha halisi ya watu weusi? 

Wachambuzi wengi wanabisha hilo na mimi naungana nao.Show ya EMPIRE inaonekana kama inamwaibisha mtu mweusi kwa kuwa show hii imeonyesha kuwa watu weusi wengi ni wauza madawa,walevi na majambazi.Pia ndani ya EMPIRE inaonyesha kuwa watu weusi wengi wametumia njia haramu za kupata kipato mpaka wanatimiza ndoto zao (Lucious Lyon na Cookie),
Pia show hii imezingua kitu kingine ambacho wachambuzi wamekiita "over potraying gay theme" katika series hii ushoga umeonekana sana kwa sababu mmoja wa wahusika wakuu Jussie Smollet (Jamal) ameigiza kama shoga (ni shoga pia kstika maisha ya kawaida).

Pia wachambuzi wameponda jinsi uhusika wa mama ulivyovaliwa,Taraji P Henson au Cookie katika EMPIRE hajacheza uhusika kama mama mweusi anavyotakiwa acheze,ila hatuwezi kumlaumu Cookie kwa sababu yeye ni mwigizaji tu lawama zote zinarudi kwa Lee Daniels producer mkuu wa show hiyo,LD alipoulizwa kuhusu ushoga katika  EMPIRE amesema kuwa ushoga umeonyeshwa sana katika series hiyo ili kuwaasaidia mashoga katika jamii ili nao waonekane kama watu wa kawaida,lakini je hizo ni tamaduni za watu weusi? 

Katika season 2 Lee Daniels ameshaanza kutuonyesha mapenzi ya jinsia moja kwa wanawake (lesbianism).Martin Luther King angekuwepo angetoa maoni gani?Malcolm X angefufuka leo na kujionea EMPIRE angetoa maoni gani? Sidhani kama wangependa kuona watu ambao wamewapigania haki zao wanawasaliti.Huu ni mtazamo wangu kuhusu Empire mmependa mziki Lee Daniels kafanya vizuri katika hilo.


No comments:

Powered by Blogger.