Breaking News
recent

PENTATONIX,WAKALI WA ALCAPELLA.

Unapoongelea makundi ya muziki ya kuimba bila beat (alcapella) utakuwa hujatenda haki kama hautowataja PENTATONIX' kundi hili lilianzishwa mnamo mwaka 2011 na vijana watatu Mitchie' Scott pamoja na mdada Kristine: wakati huo walikuwa bado wanasoma MARTIN HIGH SCHOOL ambayo ipo Texas'Marekani...

 baadaye member wawili Avi na Kevin waliongezeka' Pentatonix kipindi wapo shule wakasikia tangazo katika radio kuwa cast ya GLEE imeandaa shindano la kutafuta kundi kali la kuimba nao mziki katika series ya GLEE' Pentatonix walituma nyimbo ya Telephone ya Lady Gaga lakini hawakufanikiwa kushinda baada ya hapo wakawa maarufu shule nzima ndipo wakashiriki katika mashindano ya NBC-SING-OFF wakafanikiwa kushinda.

 Baada ya kushinda shindano hilo wakaingia mkataba na lebo ya SONY MUSIC' ndipo wakaachia vibao kama Daft Punk ambacho kilipata viewers zaidi ya milioni 150 youtube' hadi sasa PTX wana subscribers zaidi ya Milioni 9 katika chanel yao ya Youtube: Pia waliachia albamu zao kama EP' PTX-Volume 1 na 2 Pia PTXmass ambazo zilivunja rekodi billboard na kuwa albam ya nne iliyoongoza kwa mauzo nchini Marekani.

Pentatonix pia wana tunzo nyingi ila kubwa ni ya Gramy waliyopewa katika kipengere cha Best Alcapella group!!


No comments:

Powered by Blogger.