HEROES-REBORN ni series iliyorudi tena mara baada ya kuwa cancelled miaka michache iliyopita.series hii hapo kabla ilijulikana tu kama HEROES,Ika kwa sasa ilivyorudishwa tena hewani inaitwa HEROES-REBORN.
kwa ufupi series hii inaanza kwa kuonyesha kuwa binadamu wenye uwezo wa ajabu,maarufu kama "Evos" name binadamu kawaida wanaishi kwa amani tu sio kama zamani ambapo Evos walikuwa wanawindwa.Evos wapo wenye uwezo mbali mbali,kuna wenye uwezo wa kupaa,kutoa moto,kupotea,kujibadilisha sura,kugeuka wingu n.k.Evos na binadamu wanaishi kwa amani tu lakini kwa bahati mbaya mlipuko mkubwa unatokea maeneo ya Odessa,Texas nchini Marekani ambapo watu wengi wanakufa katika mlipuko huo.
Mlipuko huo unaleta ugomvi tena katika ya binadamu na Evos ambao wanahisiwa kuwa walisababisha mlipuko huo.Noah Bennet ambaye hapo zamani alikuwa anawinda Evos alikuwepo katika mlipuko was Odessa Lakini hakumbuki vizuri nini kilitokea Siku hiyo.Noah baada ya kufanya utafiti anagundua kuwa yeye mwenyewe aliomba atolewe kumbu kumbu ili asahau kilichotokea Odessa.Noah anajaribu kukumbuka non kilitokea Odessa? Na kwanin aliomba afutwe kumbu kumbu?
Wakati huo huo kuna kijana anaitwa Tomy, Tomy ana uwezo wa kupotea na kutokea sehemu yoyote ile atakayoiwaza kichwani kwake,Pia ana uwezo was kukigusa kitu au Mtu na kumpoteza aende sehemu yoyote(teleportation) ile anayofikiria kichwani kwake.Tomy anaishi na mama yake ambaye ni binadamu wa kawaida,Tomy na mama yake wanaishi kwa kuhama hama,Mara nyingi wanahama ili kuwakimbia watu wanaowinda evos.
Tomy baadae anakuja kugundua kuwa mama aliyekuwa anaishi nae sio mzazi wake baada ya kupata ajali akiwa na mama yake ambaye alipoteza damu nyingi katika ajali,Alipompeleka hospitali doctor anamwambia hawezi kumwongeze damu mama Yake kwasababu haziendani,baadae mama yake anapata nafuu na kujaribu kumwambia tomy ukweli kuhusu yeye na baba was Tomy,Tomy anakasirika na kuamua kupotea kwa hasira.
Wakati huo huo pia nchini Japan msichana Kitana anagundua kuwa ana uwezo wa kuingia kwenye video games,Kitana anagundua kuwa baba yake amenasa ndani ya game kumtoa inabidi Angie ndani ya game na panga Fulani la kisamurai,kwa bahati mbaya atanyang'anywa ndipo kwa msaada was rafiki take wanaamua kwenda nchini Marekani ili walitafute panga hatimaye wamtoe baba yake aliyenasa kwenye game.
Pia kuna jamaa anaitwa Luc yeye na mke wake motto wao aliuliwa name Evos,hivyo Luc na Mke wake in with wanaowawinda Evos na kuwaua.Baadae Luck anagundua na yeye ni Evos mwenye uwezo wa kutoa moto kwenye mikono,Luck anashindwa cha kufanya mke wake baada ya kugundua anamwacha.Watu wote hao Noah,Luck,kitana,Tomy name Evos wengine inabidi waungane ili kuiokoa dunia name balaa linalotarajiwa kuja,kilichotokea Odessa ni mwanzo tu.Balaa gan hill linakuja? Anglia HEROES REBORN ujue!!!
SERIES YA HEROES REBORN.
Reviewed by Unknown
on
13:42
Rating: 5
No comments: