JUSTIN BIEBER ALIVYONG'ARA MWAKA 2015!
Mimi sio shabiki sana wa Justin Bieber hasa katika miaka ya hivi karibuni,kidogo zamani alikuwa ananipa hamasa,lakini alipoanza kuzingua nikawa simfuatilii sana.lakini JB wa sasa ni mpya,JB wa sasa amekua,JB wa sasa ameamua kujikita kabisa katika shughuli za muziki na zimemletea mafanikio.Mwaka huu 2015 ni mwaka wa Bieber hii ni kwa sababu ya mambo yafuatayo:
1-Justin Bieber amevunja rekodi ya The Beatles,JB amefanikiwa kuvunja rekodi ya The Beatles ya kuingiza nyimbo 14 kwenye top 100 ya billboard ndani ya week moja,JB yeyr kaingiza nyimbo 17 katika top 100 ya billboard hivyo kuvunja rekodi hiyo ya kundi hilo maarufu la zamani.Rekodi hiyo ilivunjwa baada ya kukaa zaidi ya miaka 50 hata Marehemu Michael Jackson alishindwa kuivunja,imekuja kuvunjwa na kijana wa miaka 21 kutoka Canada Justin Bieber.
2-Justin Bieber amewapiku ONE DIRECTION kwa mauzo ya albamu,Novemba hii hii 1D waliachia album yao inayoitwa PERFECT Justin naye aliachia album yake inayoitwa PURPOSE,lakini ndani ya Siku chache tangu iachiwe imeuza mamilioni ya nakala na kufanikiwa kuipiku album ya 1D kwa kuuza maelfu zaidi ya nakala za 1D.
3-Justin Bieber amefanikiwa kushinda tuzo za MTV EMA AWARDS kwa mara ya tano mfululizo, JB ndiye msanii anayeongoza kuchukua tuzo za MTV EMA AWARD kipengele cha BEST MALE ARTIST,JB kachukua tuzo hiyo Mara tano mfululizo na kufanya tuzo hiyo ibadilishwe jina na kuitwa "BIEBER'S AWARD".
4-Justin Bieber kaachia vibao vikali mwaka huu ,JB kaachia nyimbo Kali sana mwaka huu ndio maana 17 kati ya hizo zipo katika top 100 ya billboard,Kibao choke cha SORRY kipo namba 2 nyuma ya kibao cha Adelle HELLO kinachoshikilia namba 1.Ukitoa hizo pia vibao vyake kama WHAT DO YOU MEAN?,PURPOSE na vinginevyo vinafanya vyema.Hakika 2015 ulikuwa mwaka wa JB kama ulivyokuwa mwaka wa Diamond hapa bongo.
No comments: