Breaking News
recent

SABABU KADHAA ZA KUMPENDA KATY PERRY!


Ukinambia nimchague msanii yoyote wa kike wa mbele ninaowakubali ntakutajia Lenka,Miranda Lambert,Beyonce kwa mbali,Adelle and the list goes on lakini siwezi nikamuacha mwanadada Katherine Perry,
Namkubali sana Katy Perry kwa sababu zifuatazo:

1-Video zake za kipekee,sijaona msanii yoyote yule duniani ambaye anaweza kumfunika Katie kwa video Kali,hakuna cha Beyonce,Rihanna wala lady Gaga,Katie ana video nzuri na za kipekee,angalia "Roar" utafikiri unaangalia movie kama TARZAN au SHEENA, pia ukicheki video kama "wide awake" ni nzuri na ya kipekee ukiichek utafikiri unaangalia movie ya ALICE IN THE WONDERLAND, mazingira mazuri na ya kuvutia,Angalia pia video yake ya "part of me" nayo ukiichek utafikiri unaangalia movie ya GI JANE,ukitoa hizo pia ana video Kali kama "California girls" na "fireworks" msanii wa kike anayeweza kumsogelea Katy Perry kwa video Kali ni Taylor Swift tu.

2.Katy Perry hana Beefs za kijinga jinga, ni Mara chache sana nimesikia Katy Perry ana ugomvi na wasanii wenzake,hata hivi karibuni alivyozinguana na Taylor bado hajaonyesha nia yoyote ya kutaka kulipa kisasi au hata kumtupia mane no makali,lakini kwa Taylor ilikuwa ishu kubwa na hadi akamtungia katty nyimbo ya "Bad Blood" lakini hadi Leo Katy perry hajalipa nyimbo hii,ingawa kulikuwa na tetesi kuwa atashirikiana na Rihanna kuachia kibao hicho.Katy Pia aliwahi kukosolewa na Adelle aliyesema kuwa Katy anapenda kuachia sehemu kubwa ya maungo yake wazi katika video zake nyingi,akaendelea kusema pia yeye anafanya muziki wake kwa ajili ya masiko ya watu na sio macho ya watu.Maneno hayo ya Adelle hayakumfanya achukiwe na Katy Perry lakini akayachukulia tu kama changamoto na akaendelea na mziki wake.

3-Nyimbo za Katy Perry zinahamasisha kufanya kitu Fulani,ukitoa nyimbo zake za mapenzi kama "unconditionally"," dark horse" "teenage dream" na nyinginezo,sikiliza nyimbo zake kama "wide awake" "walking on air" "part of me" bila kusahau "roar" zote hizi ni nyimbo za kuhamasisha pia zinatia moyo kwa wale waliokata tamaa.

4-Katy Perry ni bonge la mwanamitindo ,napenda jinsi Katy Perry anavyovaa pia anavyo badili badili style zake za nywele na zote zinamkaa vyema,Katy perry havai mavazi ya ajabu ajabu kama Lady Gaga lakini anapendeza na kuteka attention ya watu.

5-Katy Perry ana Show Kali,show nyingi za Katy perry zinakuwa gumzo,katika show ambazo alinikosha ilikuwa ni ya MTV EMA 2013 alipotengeneza


jukwaa kama ulingo na kuimba wimbo walke mkali wa ROAR.



No comments:

Powered by Blogger.