Breaking News
recent

MOVIES NA SERIES KALI ZA MUZIKI.

Hollywood wanasifika duniani kwa kutengeneza movies na series kali za maudhui mbali mbali,Hollywood wanatengeneza moviez za action,drama,horror,thriller hata comedy,kila sekta wapo vizuri that's why wanaongoza duniani kwa kutengeneza movies zenye ubora wa hali ya juu,wakifuatiwa kwa karibu na Bollywood.ukiangalia movies za kihindi [bollywood],karibia asilimia 90 za movie zina muziki ndani,tofauti na Hollywood ambao movie zao hazina nyimbo,wakitaka movie iwe ina nyimbo wanaitengeneza kivyake bila kuhusisha maudhui mengine.Zifuatazo ni baadhi ya Movies na Series kali za muziki zilizofanywa Hollywood.
1.THE SOUND OF MUSIC;Ni moja ya my all time favorite movie,Ni movie ya zamani haswa ikiwa imechezwa miaka ya sitini.Movie inamuhusu sister Maria ambaye yupo tofauti kidogo na masister wengine,yeye hupenda kutoroka na kwenda milimani kuimba na mara nyingi huchelewa misa na shughuli mbali mbali ambazo wanafanya masister,Baadae anaitwa na mkuu wa masister na kuambiwa kuwa anahitajika aende kulea watoto wa Captain flani anayeheshimika,watoto wapo sita na kila mfanyakazi anayekuja kuwalea anaacha kazi kutokana na vituko anavyofanyiwa na hao watoto,Maria baada ya kupata tabu siku za mwanzo hatimaye anawaweka sawa lakini bahati mbaya anajikuta katokea kumpenda Captain ambaye ni baba wa watoto hao,Maria atafanyeje wakati yeye ni sister...Tafuta movie hii utajua.
MARIA AKIWA NA CAPTAIN,PAMOJA NA WATOTO WAKE SABA.

movie hii ya SOUND OF MUSIC ilishawahi kushinda Oscar tano enzi hizo ni bonge la movie ingawa ni ya zamani lakini nikiitazama leo naona bado mpya.
2.SISTER ACT;ni moja kati ya movie ambazo sichoki kuziangalia,humu ndani yupo Mwanamama WHOOPI GOLDBERG maarufu kama Mama Masumbuko kwenye movie ya SARAFINA.Hii movie nayo kama SOUND OF MUSIC pia ni ya zamani,lakini yenyewe ni ya miaka ya 80 mwishoni.Inamhusu Msichana flani ambaye alikua anaimba katika klabu mbali mbali jijini las vegas kwa bahti mbaya anashuhudia mauaji katika klabu anayoimba,ili kujinusuru maisha yake anakimbilia polisi.Polisi wanaamua kumficha katika nyumba ya masister akipewa jina la uongo la Sister Marry Clarence,inabidi ajifiche humo hadi tarehe ya kwenda kutoa ushahidi mahakamani itakapofika,akiwa kwenye jumba la masister anapata shida kutokana na style yao ya maisha,baadae anapewa adhabu ya kuwa kwenye kwaya ndipo anagundua kuwa kwaya ya masister ina matatizo makubwa katika uimbaji.Sister Marry Clarence kwa kuwa ana uzoefu wa kuimba klabu ndipo anaamua kuwa choir mistress akizigeuza nyimbo za kidunia kuwa za dini,baada ya muda kwaya inaanza kupendwa na kanisa linajaa kila jumapili kuishangaa kwaya hiyo lakini ni sister mkuu pekee pamoja na polisi wanaojua ukweli kuwa Sister Marry Clarence sio Sister kweli...nini kitatokea tafuta uicheki.
3.LET IT SHINE;Ukiongelea movie za disney zilizofanya vizuri mwaka 2012 huwezi ukaisahau movie ya let it shine,nilichoipendea LET IT SHINE ni movie ambayo ukiangalia hata na mzazi wako anawez akaipenda,Movie inamhusu kijana Cyrus ambaye ni mtoto wa mchungaji.baba yake hapendi na wala hataki kusikia miziki ya kidunia hasa hasa hip hoip,bila kujua kuwa mwanae ndio mziki aupendao.Kila siku Cyrus ambaye pia ni mpiga kinanda kanisani,anaenda klabu ikiwa kama part time job yake,Mama anajua lakini baba hajui,Cyrus akiwa klabu mara nyingi huangalia mashindano ya freestyle ambayo yametawaliwa na jamaa anajiita bling kila shindano huwa anashinda,Cyrus ana kipaji kikubwa cha kuandika mistari na kutengenez midundo,kwa bahati kuna shindano la kuandika nyimbo ili itumwe kwa msanii mkubwa roxanne ambae amewahi kusoma nae wakiwa watoto,mshindi wa hilo shindano atapata nafsi ya kufanya collabo na roxanne,Cyrus wakiwa na rafiki yake Chris ambaye anapenda sana wanawake wanakubaliana kushiriki shindano hilo na kila mmoja akijigamba kumpiku mwenzie.Cyrus katika kutuma bahasha yenye cd ya nyimbo yake kwa ajili ya kushiriki shindano,anaweka picha akiwa pamoja na Chris na kuituma,bahasha ilipomfikia Roxanne anaaipenda nyimbo lakini akajua aliyetunga nyimbo ni Chris na siyo Cyrus,hapo ndipo movie inaanza kunoga...the rest tafuta uicheki kama bado.
TYLER WILLIAMS JAMES,COCO JONES NA TREVOR JACKSON.

Bonge la movie kutoka kwa DISNEY,moja ya movie iliyowapa heshima watu weusi duniani kutokana na kuwa na maadili,movie hii imethibitisha kuwa sio lazima movie iwe na mambo ya ajabu ajabu kama series ya empire,ndipo ipendwe la hasha ukitunga stori nzuri movie lazima itakubalika tu.
4.CAMP ROCK; Nayo pia imetengenezwa na disney,Camp rock ina muendelezo sequel,Camp Rock ya pili inaitwa final jam,hii movie ilibidi acheze Selena Gomez lakini kulikuwa kuna muingiliano wa ratiba Selena alikuwa ana ofa ya movie nyingine,hivyo nafasi yake akapewa rafiki yake Demi Levato.Camp Rock pia ina wahusisha jonas brothers ndugu watatu [kelvin,Nick na Joe],Inamhusu msichana Mitchie ambae na ndoto za kuwa mwanamziki mkubwa,kwa bahati kuna camp inaitwa camp rock ambayo watu huenda kujifunza muziki na kucheza,mama yake Mitchie hana uwezo wa kumudu gharama za mwanae kuishi camp,hivyo anaamua kupika vyakula na kuwahudumia watu kwenye camp,Mitchie anaenda kumsaidia lakini anawadanganya baadhi ya wasichana kuwa mama yake ni mwanamziki mkubwa kumbe mama yake ni mpishi wa camp.Pia kuna kundi maarufu la mziki linaliotwa 3 connect likiongozwa na Shane Gray,kundi hilo ndilo linalohusika na kufundisha watu mziki pamoja na kucheza kwenye hiyo camp.Siku Shane Gray kaatika pita pita zake anasikia sauti ya Mitchie akiimba,anavutiwa na wimbo aliokuwa akiimba Mitchie na kuanza kumsaka......
Bonge la movie toka kwa disney,hii movie nilikuwa naipenda mpaka nikawa nimeshika karibia nyimbo zote,nyimbo niliyoipenda zaidi ipo kwenye part 2,aliimba Nick Jonas inaitwa introducing me,hadi leo sijaisahau ndio nyimbo iliyonifanya niirudie rudie movie hii mara kadhaa.
5.PITCH PERFECT;Imechezwa na msichana Anna Kendrik ambaye alikuwa nominated kwenye tunzo za OSCAR mwaka huu,inamhusu msichana Becca ambaye ni mtaalamu sana wa kutengeneza beats mbali mbali,anajiunga na chuo cha Barden University akiwa chuoni hapo anavutiwa na kundi la wasichana tupu la mziki linalojiita the bellas,wasichana hao wanasifika kwa kuimba bila mabeat [alcapella].Anajiunga nao na kuleta ladha tofauti katika kundi hilo na kuwasidia kushinda katika mashindano ya alcapella yaliyokutanisha vyuo mbali mbali.
Niliipenda sana hii movie hasa part 2,kipande kilichonifurahisha zaidi ni pale kundi maarufu la alcapella PENTATONIX,walipoonekana,ingawa ilikuwa ni kwa muda mfupi lakini waliongeza radha flani amazing.PITCH PERFECT ni movie nzuri na yenye nyi,mbo nzuri,mtu niliyempenda zaidi kwenye hii movie ni mwanadada mwenye vituko fat amy.
6.GLEE;Katika series nzuri za muziki huwezi ukaisahau series ya GLEE ambayo ilianza mwaka 2009 may 19,mpaka march 20 mwaka 2015, ikiwa ina seasons 6.Inahusu Mwalimu wa spanish Will Schuester anajitolea kuifundisha kwaya ya shule ya William McKinley High School,yenye jina la New Directions anapata wakati mgumu licha ya kufanikiwa kuwakusanya members 12,licha ya kuwa na vipaji members wa New Directions,wanapata wakati mgumu kumudu maisha yao ya kimuziki na matatizo yao ya kijamii.

 Mwalimu Will licha ya kuwasaidia kimziki anakua mlezi mzuri wa vijana hao,akiwasidia kutimiza ndoto zao huku naye akipambana na changamoto mbali mbali za familia na maisha kiujumla,Uzuri wa glee napenda jinsi wanavyozirudia nyimbo za wasanii wengine[cover songs],na kuzifanya ziwe nzuri kuliko hata original songs.
 7.INTO THE WOODS,Ikiwa imeandaliwa kama kawaida na disney,ikichezwa na waigizaji wengin wazoefu kama Anna Kendrik ambaye kaigiza pitch perfect,pia kuna John Depp a.k.a master of disguise,Chris Pine,Emily Blunt na wengine wengi...inamhusu Mchawi ambaye anawaamulu Mwoka Mikate [baker] na mkewe,waende kumtafutia vitu flani ambavyo akivipata vyote anaweza akavunja spell aliyowekewa ambayo inamfanya awe mzee,Mwoka Mikate na mkewe hawakujaliwa kupata mtoto hivyo anawapa ahadi kuwa wakifanikiwa kumletea hivyo vitu,atawasaidia kupata mtoto wakishindwa basi atawaua....
ANNA KENDRIK au CINDERELLA KATIKA MOVIE YA INTO THE WOODS
Nilichoipendea hii movie imefanya kama series ya once upon a time,imeunganisha hadithi nyingi za kufikirika maarufu kama fairy tales na kufanya iwe hadithi moja,humu ndani kuna hadithi nyingi kama  Jack and the beanstalk,Rapunzel,Cinderella na Little Red Riding Hood.INTO THE WOODS ilifanikiwa kushinda tuzo kadhaa ikiwemo academy awards 3 na tuzo za golden globe awards 3 pia.

8.EMPIRE,Ingawa inakosolewa na wadau wengi wa filamu kuwa haina maadili na inachochea ushoga,bado empire ni series iliyowapa heshima watu weusi.Empire imezitoa jasho series kibao za wazungu kama the flash,originals,csi,i zombie na nyinginezo kwa kuwa na viewers wengi  duniani,series hii inamhusu lucious lyon mmiliki wa kampuni ya muziki ya Empire,baada ya mke wake kukaa jela kwa miaka kadhaa anatoka akidai shea za kampuni kwa sababu pesa zilizohusika kujenga kampuni zilitokana na madawa ya kulevya aliyoyauza yeye,Lucious ana watoto watatu Hakeem anayependa hip hop,Jamal ambaye anaimba rnb lakini ni shoga,jambo ambalo linamuudhi Lucious na kujikuta akimchukia mwanae huyo,mwanae mwingine hana kipaji cha mziki lakini ni mzuri katika management ya kampuni kwa kuwa ni msomi...series nzima inaonyesha visa mbali mbali vinavyofanywa na familia hii wakiwa na upinzani mkali wa kugombania kampuni ya muziki ya empire.
 Nilchopenda katika series ya Empire hasa season 1,Ni nyimbo mbali mbali hasa nyimbo ya Hakeem ya drip dripity drop,pamoja na keep your money ya Jamal,bila kusahau conqueror ikiimbwa na Jamal pia.Pia nimevutiwa na performance ya Taraji P. Henson maarufu kama cookie,alicheza vizuri sana uhusika wake mpaka akawa nominated EMY AWARDS lakini nashangaa kwanini hakuwa nominated kwenye tuzo za OSCARS..Dah kweli OSCAR AWARDS kuna ubaguzi...anyway hata kama hajapewa she is the best.
9.HIGH SCHOOL MUSICAL,Kati ya movie kali a muiki katika historia ya disney,nahisi hii hapa inaashika namba moja,hii inamhusu kijana Troy Bolton ambaye ni nyota wa kikapu shuleni kwake akiwa katika team ya wildcats,mara baada ya kukutana na msichana Gabriela maisha ya Troy yanabadilika anajikuta akipenda music,familia hasa baba yake anajaribu kumuweka mbali na music,lakini Troy anajaribu kubalance maisha yake katika kikapu na music hatimaye mwisho wa siku anafanikiwa katika vyote.

naikubali sana HIGH SCHOOL MUSICAL,anayenifurahisha sana ni mwanadada sharpey ambaye anafanya juu chini kujihakikishia anampataTroy,wakati Troy moyo wake upo kwa msichana Gabriella.
Hio ndio orodha yangu ya movies na series kali enye maudhui ya music,nyingine ni hairspray,lemonade mouth na,joyful noise.tchaooo..stay tuned for our upcoming posts.....





No comments:

Powered by Blogger.