Kwa mashabiki wa movie za FAST & FURIOUS likuwa huzuni kubwa pale mwigizaji Paul walker alipofariki dunia katika ajali ya gari.Yafuatayo ni baadhi ya mambo ambayo inawezekana ulikuwa huyajui mwigizaji Paul Walker.
1.paul Walker alikuwa anapenda sana kuendesha magari kwa kasi na mara kadhaa amewahi kushiriki mashindano ya magari "Redtime racing series" akitumia gari yake aina ya BMW.
2.Paul walker alikuwa ana moyo wa kusaidia watu alianzisha mfuko uitwao"Reach Worldwide" uliokuwa unalenga kutoa msaada kwa nchi zilizokumbwa na majanga asili.Pia Paul Walker aliwahi kumsaidia Veterani mmoja wa kijeshi aliyekuwa dukani akitafuta pete ya ndoa kwa aajili ya mke wake.Paul alimwambia muuza duka kuwa yeye ndiye atakayelipa bili ya veterani huyo.
3.Paul Walker alikuwa rafiki mkubwa sana kwa waigizaji wenzake Vin Diesel Na Tyrese Na walikuwa wakimuita Paul jina la utani "Pablo".
4.Paul walker alikuwa ana mkanda wa brown wa sanaa ya mapigano ya kibrazili iitwayo "ji jitsu" na alikuwa anakaribia kupewa mkanda mweusi kabla hajafa hivyo siku ya mazishi yake mwalimu wake aliuweka mkanda mweusi juu ya jeneza kama ishara ya heshima na kumbu kumbu.
5.Paul Walker aliaanza kuonekana katika televisheni tangu akiwa mdogo mnamo miaka ya 70's Paul Walker alionekana katika tangazo la la kutangaza Pampers.
6.Mke wa Vin Diesel alipojifungua mtoto wa kike mtoto huyo alipewa jina la "Pauline" Vin Diesel alimpa mwanae jina hilo kama ishara ya kumkumbuka na kumuenzi rafiki yake Paul Walker.
7.Paul Walker aliigiza movie yake ya kwanza mwaka 1985 wakati huo paul walker alikuwa na umri wa miaka kumi tu.Movie hiyo ilikuwa inaitwa MONSTERS IN THE CLOSET.
MAMBO USIYOYAJUA KUHUSU MAREHEMU PAUL WALKER.
Reviewed by
Unknown
on
01:57
Rating:
5
No comments: