Taraji P Henson au "Cookie" katika series ya EMPIRE pia anajulikiana kupitia kazi nzuri alizofanya katika movie za KARATE KID Na THINK LIKE A MAN pia kupitia series ya PERSON OF INTEREST.
Yafuatayo ni baadhi ya mambo ambayo inawezekana ulikuwa huyajui kuhusu mwigizaji huyu.
1.Taraji ana mtoto mmoja wa kiume aitwaye Marcel. Marcel alizaliwa mwaka 1995 baba yake Marcel aliuliwa mwaka 1997.
2.Taraji ni mmoja kati ya watu ambao wanatetea haki za wanyama.Taraji hapendi na hawezi kuvaa nguo yoyote ile iliyotengenezwa kwa ngozi ya mnyama.
3.Taraji alianza kuonekana katika series ya PARENT HOOD wakati huo alikuwa na miaka 26 lakini katika episode aliyoonekana aliigiza kama binti wa miaka 16.
4.Jina la "Cookie" analolitumia kwa sasa katika series ya EMPIRE lilishawahi kuwa jina la utani alilokuwa anaitwa na wenzake kipindi bado anasoma chuo.
5.katika series ya EMPIRE Taraji anaupenda wimbo wa "You are so beautiful" Taraji anasema anapenda ujumbe uliokuwepo kwenye nyimbo hiyo.
6.Taraji alianza kusoma mambo ya science katika chuo kimoja huko Calfornia lakini baadae alibadili kozi na kusomea mambo ya sanaa.
7.Taraji anajua sana kupika.Mwimbaji Marry J Bridge anayakubali sana mapishi ya Taraji na karibia kila sikukuu ya shukrani "thanksgiving" Marry J Bridge huwa anaenda nyumbani kwa Taraji Kwa aajili ya kula chakula cha jioni.
MAMBO USIYOYAJUA KUHUSU TARAJ P HENSON "Cookie" WA EMPIRE.
Reviewed by
Unknown
on
10:04
Rating:
5
No comments: