Breaking News
recent

HII NDIO VERSE YA KENDRICK ILIYOLETA BALAA ULIMWENGU WA HIP HOP.

Hapo kabla Kendrik Lamar nilikuwa sijawahi msingatia sana' nyimbo yake ya "bitch dont kill my vibe" ilinivutia lakini bado nikawa namchukulia kendrik kama rapper wa kawaida tu: Mwaka huu ndio nimeanza kumfuatilia Kendrik na kumkubali alinivutia jinsi alivyo-rap katika Bad Blood ya Taylor Swift Pia Katika Classic Man remix ya Jidenna: 

Hapo ndipo nikaanza kudownload nyimbo zake za zamani na nikajua jinsi gani huyu jamaa alivyokuwa mkali: Miaka miwili iliyopita mwezi August Big Sean alimshirikisha kendrik katika nyimbo ya "Control" hapo ndipo Kendrik alipoimba verse kali na ilizungumziwa na bado inazungumziwa hadi leo;kendrik katika verse hiyo alijitapa kwa kusema yeye ndiye mfalme wa jiji la New York na akawataja mastar kama Nas,Drake,Pusha T,Meek Mill na wengine wengi kuwa wakae vizuri kwa sababu amekuja kuwapoteza katika game.

Kendrik pia alijiita kizazi cha Tupac katika verse hiyo.Siku chache baada ya nyimbo hiyo kutoka mastar kibao waliizungumzia,Kama vile Uncle Snoop,P.didy,Nas,Asap Rock,T.I,Tyga,Big Sean hadi Comedian Kevin Hurt.Wengi walisema verse hiyo ni diss kwa wasanii wote waliotajwa humo na wengine wakamtetea kendrik kwa kusema kuwa hakum-diss mtu bali alikuwa anawaonya tu ma-rapper wengine wakae chonjo kwa sababu yeye ni moto wa kuotea mbali katika anga za Hip Hop.                                                                 
feel design
kendrik's verse

No comments:

Powered by Blogger.