Breaking News
recent

USHAURI WANGU KWA BONGO MOVIES.

Kwa sasa movie za kibongo zinajitahidi kufanya vizuri ndani na nje ya nchi,hii ni kutokana na juhudi za wadau mbali mbali nchini na marehemu Steven Kanumba,mimi binafsi movie za kibongo nilizoangalia zinahesabika  lakini licha ya kuzitazama chache nimeona makosa mengi ambayo inabidi yarekebishwe mara moja.Ushauri wangu kwa wadau na waigizaji wa bongo movies ni kujitahidi kuboresha mambo yafuatayo:

http://www.bongo5.com/wp-content/uploads/2013/09/c4fec086fd9f11e291ae22000ae9112d_7.jpg

1.Kuboresha movie za vichekesho:Movie za comedy bongo zina vichekesho vya maneno kuliko vitendo,kwa mfano mzungu ukimwambia aangalie MIZENGWE hatafurahia sio tu kwa kuwa lugha haielewi Bali pia haoni matendo ya kufurahisha,lakini ukimchukua MTU ambaye Haelewi kiingereza ukamwekea movie kama MR BONES,MR BEAN au CHARLIE CHAPLIN lazima afurahie kwa sababu anaona matendo yanayomfurahisha.
 

2.Kama movie inaigwa toka nje basi iboreshwe,wabongo wana mtindo was kuiga movie toka nje kwa mfano Nigeria,kuiga so kit kibaya Ila sio una-copy na ku-paste,wahindi (BOLLYWOOD) wanaiga movie toka marekani (HOLLYWOOD) lakini wanaboresha,kwa mfano movie ya director Stephen Spielberg ya ET iliigwa na wahindi wakatengeneza KOI MIL GAYA maarufu kama KRISH 1,lakini hadi Leo movie ya ET sio maarufu kama ya KRISH ingawa yenyewe ndio original.
 

3.kuongeza u-serious katika kutengeneza movie Zao,wabongo wanakurupuka tu kutengeneza movie,movie inaweza ikatengenezwa ndani ya miezi miwili tu,tofauti name wenzetu kwa mfano movie ya AVATAR ilianza maandalizi ya kutengenezwa tangu mwaka 1999 lakini ikatoka mwaka 2010.Kama James Cameroon director was movie hiyo alitulia miaka yote hiyo kutengeneza movie kwanini akina JB,Ray na wengineo washindwe.Pia u-serious unahitajika pia wakati was kutengeneza movie,kwa mfano movie ya BANG BANG ya Hritik Roshan na Katrina kaif kipindi inatengenezwa waigizaji hao waligomewa kuja na simu eneo la ku-shoot movie hiyo.Mambo kama hayo yanawezwa kuigwa na ma-director wetu nchini name hatimaye kukuza filamu nchini.
 

4.Waigizaji wawe tayari kujitoa ili kuboredha kazi Zao,wabongo wajitahidi kutumia gharama kuandaa kazi Zao il I zije kuwalipa,chukulia mfano msanii kama Diamond alikuwa tayari kuumia kuingia gharama kutengeneza video nzuri,na kwa sasa ni msanii wa kimataifa,ukiangalia HOLLYWOOD Brad Pitt na Angelina Jolie walifulia kipindi wanatengeneza movie ya WORLD WAR Z,fikiria waigizaji wakubwa kama hawa walikubali kuingia gharama kubwa kutayarisha movie hiyo ingawa walipata misukosuko na hasara kipindi wanatengeneza movie hiyo.kuna kipindi waliibiwa vifaa wakiwa location,licha ya kuingia gharama kununua tena vifaa hivyo hawakukata Tamaa na movie hiyo ilipoingizwa katika box office wiki ya kwaza tu wakawa wamerudisha gharama zote za movie hiyo.
 

5-Waboreshe soundtrack za movie,movie ili iwe tamu Lazima soundtrack iwe "catchy",yani imvutie mtazamaji kuisikiliza kutokana na scene inayoendelea katika movie,sio lazima kila scene ya mapenzi usikie nyimbo ya WEST LIFE sisi wenyewe tunaweza tukatengeneza soundtracks zetu,chukulia mfano movie za kinigeria huwa wanna soundtracks flani hivi amazing.Movie za Nigeria utasikia nyimbo flani za asili zinapigwa kutokana na scene inayoendelea kama no ya kusikitisha utasikia nyimbo ya huzuni,na kama ya kufurahisha utasikia nyimbo ya furaha.Soundtrack nayoikubai hadi leo hii ni ya movie za MISSION IMPOSSIBLE ni bonge la soundtrack na linaendana na kashi kashi ya kwenye movie.
 

6.Wajitahidi kuongeza ubunifu,utakuta movie ya kibongo ambayo ingeweza kujitosheleza part 1 pekee ina part 2.Ukiangalia movie za Hollywood kama ina part 2 basi ujue part 1 ilijitosheleza na Wakati mwingine haukutegemea kama itatoka.Pia wabongo tujitahidi kutengeneza movie hata kuhusu matukio ya kihistoria katika nchi kwa mfano vita ya maji maji,au tukatengeneza movie kuhusu mashujaa wa zamani kama mkwawa,najua ni gharama lakini ukitaka kitu kizuri lazima ukubali uumie,Pia hapa Tanzania kuna Animators wengi tu,tunaweza kuwatumia hao kutengeneza movie nzuri ya Animation itakayofanya vizuri sokoni.
 

Ni huu tu ushauri Wangu kwa wadau name waigizaji wa Bongo movies. Mungu ibariki TANZANIA Mungu bariki BONGO MOVIES.




No comments:

Powered by Blogger.