Breaking News
recent

JAMES BOND NA SIFA ZAKE.

 Ilikuwa jumapili ya tarehe 29 November nilikuwa nafurahi na wenzangu nikisherekea siku yangu ya kuzaliwa,tangu asubuhi ya siku hiyo nilikuwa najiuliza,nifanye nini ili kusherekea birthday yangu,blogger mwenzangu Prosper akanambia...dude go to the movies...,nikawaza nikaona wazo lake lipo poa.Baadaye jioni nikiwa chuo maeneo ya UDSM,washikaji wakaja room na tukasherekea siku hiyo muhimu,baada ya shamra shamra za hapa na pale wana wakaniuliza vipi leo huendi kutembea,wakanishauri niende kuogelea,nikakataa nikawaambia..guys am going to the movies...,Nikafunga safari hadi Mlimani City mall nikajisogeza pande za CENTURY CINEMAX,siku hiyo walikuwa wanaonyesha movie zifuatazo BRIDGE OF SPIES,HOTEL TRANSLAVANIA 2,HUNGER GAME MOCKINGJAY 2 na SPECTRE Movie ya James Bond iliyonivuta kuandika makala hii.Nikaamua kuchagua SPECTRE nikakata zangu tiketi na kuzama ndani kuangalia movie hiyo,nilivyokuwa naingalia ndipo nikapata kujua movie za James Bond zipoje na James Bond ana sifa gani.    Tuangalie kwanza historia za movie za James Bond.James Bond ni mhusika wa kufikirika aliyebuniwa na mwandishi wa novels IAN FLEMING mwaka 1952,ambaye aliandika novels 12 baada ya kufariki kwake mwaka 1964,waandishi mbali mbali waliendeleza stori za JAMES BOND Pia waigizaji 7 wameigiza filamu za JAMES DOND zipatazo 26.Jina la siri la JAMES BOND ni 007 FLEMING amembuni JAMES BOND kuwa ni mpelelezi wa siri wa serikali au spy,jamaa fulani mrefu,handsome,anapenda wanawake,kucheza kamari pmoja na magari ya kifahari.Movie ya kwanza ya JAMES BOND ilichezwa mwaka 1954 ilijilikana kwa jina la DR NO ikiigizwa na Mmarekani BARRY NELSON.JAMES BOND wengine walioigiza ni DAVID NIVEN, GEORGE LAZENBY, ROGER MOORE, TIMOTHY DALTON, PIERCE BROSNAN na DANIEL CRAIG ambaye ndiye kashikilia uhusika wa JAMES BOND katika miaka ya karibuni.Baada ya kuangalia sana movie za JAMES BOND nimegundua kuwa JAMES BOND inabidi awe na sifa zifuatazo;                           

 

 

   1.JAMES BOND lazima awe anajua kutumia gadgets,James Bond lazima awe anajua kutumia vizuri gadgets za kipelelezi kama yale magari,saa zenye mabomu na vifaa vingine vingi,kama tulivyomuona GRAIG DANIEL kwenye SPECTRE alivyoweza kutumia gadgets zake kama saa kujiokoa pale alipozidiwa na maadui.

 
BAADHI YA GADGETS ZA JAMES BOND
2.JAMES BOND lazima awe WOMANIZER, kwa wapenzi wa movies za 007 nadhani wanajua jinsi JAMES BOND anavyopenda wanawake,kwa movie moja JAMES BOND anaweza akalala na wanawake wanne hadi sita,ila kati ya hao kuna ambaye humvutia na kuamua kubaki nae hadi mwisho wa movie.                  

BAADHI YA WANAWAKE WALIOLALA NA JAMES BOND
3.JAMES BOND Lazima awe MJANJA, JAMES BOND lazima ajue kujiongeza mwenyewe ikitokea mission imebuma,kama kwenye SPECTRE baada ya kukamatwa JAMES BOND alitumia vizuri gadget yake ya saa kujiokoa na maadui,pia alikuwa hana back up katika mission yake lakini akaifanya vizuri.    

  4.JAMES BOND lazima awe GENTLEMAN,Siri ya JAMES BOND kupendwa na wanawake ni jinsi ambavyo anawasaidia,JAMES BOND yupo tayari aweke maisha yake hatarini kwa aajili ya mwanamke au wanawake anaowapenda,pia katika mavazi mara nyingi hupendelea kuvaa tuxedo au suti ya aina yoyote ile.
baadhi ya wanawake ambao walibahatika kweli kupendwa na JAMES BOND
5.JAMES BOND lazima awe vizuri in GUN AND PHYSICAL COMBAT, JAMES BOND lazima ajue kutumia silaha kama bunduki na bastola kwa ufasaha na pia awe anajua kupigana kwa ufasaha,kama tulivyomuona JAMES BOND wa sasa DANIEL CRAIG alivyomudu hivyo vyote viwili kwenye SPECTRE.

No comments:

Powered by Blogger.