Breaking News
recent

WABONGO WANAOWEZA KUFANYA KAZI HOLLYWOOD.

Unapoongelea HOLLYWOOD ni ndoto kwa mwigizaji yoyote yule duniani ambaye anajielewa anatamani kwenda na kufanya kazi zake za sanaa.Hadi leo hii Tanzania bado haina mwigizaji ambaye kafanya kazi Hollywood wenzetu kenya wanajivunia Lupita ambaye alishinda hadi tuzo za OSCAR na alibahatika kufanya kazi na waigizaji wakongwe kama Idris Elba.Kwa Bongo marehemu Kanumba alikuwa kidogo anatuonyesha mwanga lakini hadi anafariki hakufanikiwa kufanya kazi maeneo ya Hollywood,Jimbo la Calfornia kitongoji cha Los Angeles.HOLLYWOOD ili ufanye kazi unahitaji vitu viwili tu ambavyo vinamata LOOKS and TALENT, HOLLYWOOD ukiwa una muonekano mzuri wa kibiashara utapata kazi hata kama huna kipaji,lakini pia ukiwa una kipaji halisi cha kuigiza lazima utapewa nafasi tu.Wafuatao ni wabongo  ambao angalau wanaweza wakakidhi vigezo vya kufanya kazi HOLLYWOOD.                 

1.IDRIS SULTAN,Idris ni kijana ambaye amejizolea umaarufu mara baada ya kushinda BIG BROTHER 2014,Ni mmoja kati ya celebrities wachache ninayemkubali Tanzania,Idris ana kipaji cha kufanya stand up comedy,Idris ana nia ya kwenda HOLLYWOOD,uwezo wa kwenda HOLLYWOOD na ndoto pia anazo,Idris anatamani sana kuwa kama Trevor Noah na Kevin Hart na ukimtazama kwa jicho la pili utagundua kuwa ana uwezo wa kuwafikia.

Idris akiendelea hivi hivi anaweza akaleta mapinduzi makubwa sana ya sanaa hapa Bongo kwa sababu hadi sasa ana mpango wa kufanya tv show katika BET,akifanikiwa hilo ni mwanzo tu wa kuwapaisha wabongo level za kimataifa.  

2.WEMA SEPETU,anavyo vyote looks and talent ambavyo vina mata HOLLYWOD kilichobaki ni kwa yeye tu kuongeza juhudi na ubunifu katika kazi zake za sanaa.azitengenezeee soko la kimataifa hatimaye aweze kupata gig la maana na kufanikiwa kufanya kazi pande za Obama.

Wema ajitahidi na kutudhihirishia kuwa kweli yeye ni tanzanian sweetheart atufurahishe wabongo kwa kufanya jitihada na hatimaye siku moja awe katika level za akina Angelina jolie na Megan Good.

 3.HAMISA MOBETTO,huyu mdada she is cute as hell na Hollywood wanapenda wasichana wazuri hata wawe na kipaji au wasiwe nacho

mwanamitindo huyu akiamua kujitosa HOLLYWOOD anaweza akapata gig ya maana kwa sababu ana uzuri ambao unahitajika sana HOLLYWOOD ili mtu apate nafasi adimu ya kufanya kazi huko.

 4.ELIZABETH MICHAEL,anajulikana zaidi kwa jina la lulu huyu dogo nae kama wema tu she has looks and talent vitu viwili muhimu kufanikiwa HOLLYWOOD akiongeza umakini katika kazi zake za sanaa pamoja na ubunifu.

akiongeza hivyo basi miaka kadhaa mbele anaweza akaibukia HOLLYWOOD
ana uwezo wa kufanya hivyo anahitaji tu jitahada na mtu sahihi wa kumuongoza.

5.VYONNE CHERRY au monalisa,katika wanadada naowaheshimu hapa Bongo katika tasnia ya filamu Monalisa namba 1,Monalisa ana kipaji haswa cha kuigiza na kama likitokea zali la HOLLYWOOD atafaa kweli kwa sababu ana kipaji halisi.

 anglia movie kama SABRINA na GIRLFRIEND uone kipaji maridhawa cha mwanadada huyu..much respect kwake.

hakika tasnia  ya filamu haitakuwa na shukrani isipomtaja Monalisa katika orodha ya waasisi wa BONGO MOVIES. 


6.JOTI,Unaweza ukashangaa kwanini nimemuweka Joti hapa na kuwaacha wasanii wengine kibao wa Bongo,ni hivi..angalia jinsi Joti anavyoigiza angalia jinsi anavyokuwa mbunifu na hizo ndizo sifa za comedian bora.

 

Joti yupo flexible kama mwigizaji wa Marekani EDDIE MURPHY ambaye naye kama joti anaweza akacheza uhusika kibao ndani ya movie moja,anaweza akawa mzee,mtoto,mama,bibi au hata babu na zote akazimudu vizuri.

Joti anaweza akafanya kazi vizuri HOLLYWOOD na kufuata nyayo za Wayans,Eddie Murphy,Martin Lawrence na Wengineo.

7.IRENE PAUL, huwa nafurahi sana napoona jina lake kwenye screen kwa sababu najua jinsi anavyojua,anaigiza kila mazingira ukitaka awe wa mjini anakuwa wa mjini haswa ukitaka awe wa tkilocal anakuwa localized haswaa.

na yeye pia ana vyote looks and talent angeweza kufanya vizuri HOLLYWOOD aendelee kukaza kibongo bongo hatimaye aweze kujulikana nje pia ya Tanzania na Africa kwa ujumla.
MUNGU IBARIKI SANAA YA BONGO,MUNGU IBARIKI TANZANIA.

No comments:

Powered by Blogger.