Breaking News
recent

TREVOR JACKSON ANAVYOIGEUZA MOVIE YA LET IT SHINE KATIKA MAISHA HALISIA.


TREVOR AKIWA KATIKA TUZO ZA MTV AWARDS 2O15

Ukinambia nikutajie albamu kali mwaka huu,ntakutajia 1889 ya Taylor Swift,PURPOSE ya Justin Bieber,TO PIMP A BUTTERFLY ya Kendrik Lamar,PERFECT ya ONE DIRECTION...Lakini sitoweza kuisahau albam ya IN MY FEELINGS ya kijana Trevor Jackson.TREVOR HOWARD LAWRENCE JACKSON ndio jina lake halisia,amezaliwa August 30,1996 maeneo ya INDIANAPOLIS nchini Marekani.Trevor ni mwimbaji,mwandishi wa nyimbo,mwigizaji na pia ana kipaji cha kucheza.Kaonekana katika movies na series mbali mbali lakini zilizompa umaarufu ni LET IT SHINE na THE LION KING pia series za COLD CASE na HARRS LAW.Mnamo mwaka 2012 alishinda tuzo ya YOUNG ARTIST AWARD kipengele cha BEST PERFORMANCE IN A TV SERIES.

COVER LA MOVIE YA LET IT SHINE
Ukiangalia katika movie ya LET IT SHINE Trevor ameigiza kama Kris kijana ambaye hana kipaji hivyo anamtegemea rafiki yake Cyrus aambaye anajua kuimba,amsaidie katika shughuli zake za mziki ili amvutie msichana Roxanne.Movie hii ukimtoa Trevor imechezwa na Coco Jones Pamoja na Tyler Williams James au TRUTH.Lakini katika maisha halisia Trevor amewaacha mbali sana Coco na Tyler ambao nao wanafanya shughuli zao za  muziki.Kwa upande wa Coco kafanya ngoma kadhaa pia na baadhi ya cover songs,lakini bado hajafanikiwa sana.Tyler nae kaachia ngoma kadhaaa zimejitahidi lakini sio sana,yeye amejikita zaidi katika filamu.Trevor ambaye kwenye LET IT SHINE alionekana kama ni TRUTH fake,kwenye maisha ya kawaida amejaribu kuigeuza hii movie na kuonekana kweli ana kipaji halisi kuliko hata wenzake ambao kwenye movie wameonekana wana vipaji.
COVER LA ALBAM YA TREVOR JACKSON
Trevor kwa sasa anakuja juu na watu wameshaanza kumfananisha na Chris Brown au Trey Songs kutokana na style yake ya kuimba.Mara ya kwanza kujua kuhusu albam hii niliiona katika page ya instagram ya mpenzi wa Trevor,Zendaya nikaingia katika link iliyokuwa katika bio yake na kudownload albam nzima,track ya kwanza ikanivutia,ya pili,ya tatu nayo hatimaye albam nzima nikaipenda,Tyler ambaye kwenye movie anaonekana star hajafanya lolote la maana kwa mwaka huu ingawa kajitahidi katika anga za filamu,Trevor ambaye kwenye movie alionekana boya ndiye ana kipaji zaidi katika maisha halisia,sisemi kuwa Tyler hana kipaji,la hasha ila tu akubali kwa miaka ya karibuni Trevor anazidi kupanda chati katika muziki na filamu pia.
TREVOR AKIWA NA MPENZI WAKE ZENDAYA KATIKA UZINDUZI WA ALBAM.
Trevor mwaka huu licha ya kufanya vizuri katika anga za mziki alijitahidi pia katika filamu ambapo ameonekana katika series na movies kadhaa,ila aliwavutia wengi pale alipokuwa guest star katika series ya CASSIE UNDERCOVER ambayo imeigizwa na mpenzi wake Zendaya.Trevor alionekana katika moja ya episodes pamoja na mpenzi wake Zendaya wote wakiigiza kama spies.Trevor kawafunika vibaya wenzie katika movie ya LET IT SHINE,na katika maisha halisia naweza nikasema Trevor ndiye truth haswaaaa.

No comments:

Powered by Blogger.