mwaka 2015 ndio huu unakata,Tunakaribia kuingia mwaka 2016....lakini kabla hatujaibukia mwaka huo ni vizuri kujikumbusha yaliyojiri mwaka huu.Hapo chini ntakuletea watu waliofanya vizuri katika mwaka 2015,TAHADHARI ni kuwa hii orodha nimeindaa kutokana na mtazamo wangu hivyo usishangae kuona baadhi ya vitu au watu wanakosekana..this is MY BEST OF 2015.
1.BEST MOVIE Ni Mad Max Furry Road,kwa mwaka huu hakika sijaona movie kali kama MAD MAX ni bonge la movie,hapo kabla tumeshawahi kuiandikia makala posts kadhaa nyuma,nilipitia pia chambuzi nyingi kuhusu hii movie na wengi wanaisifia,Mad Max ni mfano halisi wa movie ya ACTION inavyobidi iwe
kama hujaangalia hii movie,mwaka ndo huu unaishia fanya mishe uipate kwa sababu utakuwa umekosa movie bora na yenye creativity ya hali ya juu
2.BEST SERIES Ni Quantico,bonge la series kutoka kwa kampuni ya ABC,hapa katika kuchagua series bora ya mwaka nilijishauri sana kwa sababu mwaka huu 2015,zimetoka series kali nyingi sana lakini kwangu mimi Quantico ni kali zaidi.
Ni vizuri kuona mrembo toka BOLLYWOOD anafanya vyema pande za HOLLYWOOD hii series nilichoipendea ni ina twists kali sana,mtazamaji huwezi ukatabiri nini kitatokea,storyline imesimama vyema actors wameitendea haki.
3.BEST SONGS ni locked away na fight song,mwaka 2015 kulikuwa na nyimbo kali sana ila kwa upande wangu nyimbo ya locked away ya Rock City na Adam Levine ilisimama zaidi,nyimbo hii imechanganya raggae na pop,binafsi huwa naamini Adam Levine kiongozi wa kundi la maroon 5 akishirikishwa katika nyimbo huwa haaribu yaani anainyoosha kweli,na nyimbo hii pia alifanya yake
Nyimbo nyingine kali ni fight song ya mwanadada Rachel Platen,nilikuwa sijawahi kumsikia mwanadada huyu mpaka pale alipoachia ngoma hii kali inayohamasisha hii ngoma niliifananisha kidogo na roar ya katty Perry kutokana na maudhui yake yanaelekana kidogo,pongezi kwa Rachel the song was hot.
4.BEST COME BACK SONG Ni hello,Adelle alikuwa kimya sana kwa muda mrefu ndipo akarudi kwenye game,na kuachia kibao cha hello kilichofanya vyema na kuvipiku vibao kama sorry na what do you mean katika chati za Billboard vibao vyote viwili ni vya msanii Justin Bieber
5.BEST ARTIST Ni Justin Bieber,mwaka huu 2015 ulikuwa wa JB vibao vyake vimefanya vizuri,albam yake ya PURPOSE inafanya vizuri pia sokoni.
6.BEST ALBUM Ni Purpose Ya Justin Bieber,Yeah ni mwaka wa JB huu,Kuna album nyingi sana zimetoka kama TO PIMP A BUTTERFLY ya Kendrik Lamar,1989 ya Taylor Swift,IN MY FEELINGS ya Trevor Jackson na PERFECT ya One Direction ambayo angalau ilikuwa inaifukuzia PURPOSE kwa mauzo.
7.BEST GROUPS ni One Direction na Little Mix,licha ya kumpoteza mwenzao ambaye aliamua kujitoa,Zayn Malik.Kundi halijapoteza morale siku chache baada ya Zayn kujitoa wakaachia ngoma ya drag me down iliyofanya vizuri.Pia wameachia album yao ya PERFECT ambayo inaifukuzia album ya Justin Bieber kwa mauzo.
kwa upande wa wanawake makundi mawili yalinivutia zaidi,ambayo ni fifth harmony na little mix yana upinzani mkali sana haya makundi,pia mashabiki wa pande zote hawapatani anyway kwa upande wangu little Mix wamenikosha sana mwaka huu hasa na kibao pamoja na video yao ya black magic.
MY BEST OF 2015.
Reviewed by
Unknown
on
03:32
Rating:
5
No comments: